Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Kindamba: Tujitokeze kuchanja, karibuni Njombe
Habari Mchanganyiko

Kindamba: Tujitokeze kuchanja, karibuni Njombe

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Njombe (RC) nchini Tanzania, Waziri Kindamba amewaomba wananchi kujitokeza kupata chanjo ya virusi vya korona (UVIKO-19) kwani haina tatizo kwa wanaochanjwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

RC Kindamba amesema hayo leo Alhamisi, tarehe 31 Machi 2022 wakati akizindua kongamano kubwa la kujadilia masuala mbalimbali ya afya. Kongamano hilo limeandaliwa na wadau mbalimbali wa kiserikali na binafsi.

Kongamano hilo linafanyika kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge Kitaifa zitakazofanyika Jumamosi hii tarehe 2 Aprili 2022 katika Viwanja vya Sabasaba mkoani humo.

Kindamba amesema, mara baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe moja ya jukumu alilopewa ni kwenda kusimamia uchanjaji, “na mimi tayari nimekwisha kuchanjwa, achaneni na maneno ya huko kuwa ukichanja unakuwa zombi, ingekuwa hivyo basi mimi nisingekuwa hapa.”

Amesema, kwa takwimu zilizopo mpaka sasa wananchi waliokwisha kuchanjwa Njombe ni 35,294 sawa na asilimia 10 wamechanjwa na lengo ni kufikia asilimia 70.”

Kuhusu kongamano hilo amewaomba washiriki kutoa mawazo yatakayochangia kuboresha sekta ya afya.

“Ni wakati mwafaka kupaza sauti ya kupambana na magonjwa ukiwemo UVIKO-19 ili kujadiliana kupitia kongamano hili la afya ili kuibua mipango mizuri, kuchochea mabadiliko kwa wananchi ili kuzingatia njia sahihi ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko,” amesema RC Kindamba.

Amesema, kauli mbiu ya mwaka huu ya Mbio za Mwenge itakuwa “Kimbiza Korona na Mwenge wa Uhuru, Chanja sasa” inapaswa kuwa chachu ya wananchi kuchanja.

Aidha, amewapongeza waandaaji wa kongamano hilo zikiwemo taasisi binafsi kama Chuo cha Kikuuu cha Mryland Baltimore (UMB), Benki ya NMB na Henry Jackson Foundation Medical Research International (HJFMRI).

RC Kindamba aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) amesema maendeleo yoyote yale yanategemea afya bora za wananchi ili kuwawezesha kuchangia katika shughuli mbalimbali.

“Niseme tu, Njombe inakwenda kupaa, tuko tayari na upaaji wa Njombe itategemea sisi tunashikama mikono,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!