March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kinda wa Leicester City yaiongeza nguvu Serengeti Boys

Ben Antony Starkie, kulia kinda anayeichezea timu ya Leicester City ya England

Spread the love

MTANZANIA anayechezea klabu ya Leicester City, Ben Antony Starkie anatarajiwa kutua leo nchini 26 Julai, 2018 kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys.’ Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Starkie mwenye umri wa miaka 16 ataungana na wenzake kwenye kambi hiyo kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya vijana wenye chini ya umri wa miaka 17, maarufu kama CECAFA zone qualification yanayotarajiwa kufanyika kati ya Octoba 2018 – Aprili 2019.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeamua kumjumuisha kikosini kinda huyo kutokana na kutekeleza maagizo ya mkurugenzi wa michezo Dk. Yusuph Singo aliyetaka kusakwa kwa vipaji vya watanzania wanaocheza nje ya nchi ili kuja kusaidia Timu ya Taifa.

Agizo hilo limetoka baada ya kuona idadi kubwa ya wachezaji wenye asili au wazaliwa wa Afrika kukipiga katika baadhi ya timu za Taifa barani Ulaya kwenye michuano ya kombe la Dunia iliyomalizika hivi punde.

error: Content is protected !!