Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kinana:JNHPP ni utekelezaji wa Ilani ya CCM
Habari za Siasa

Kinana:JNHPP ni utekelezaji wa Ilani ya CCM

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amesema ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP), ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho. Anaripoti Selemani Msuya, Rufiji, Pwani…(endelea).

Kinana amesema hayo leo Alahamis tarehe 22 Desemba, 2022, wakati akitoa salamu za CCM kwenye hafla ya zoezi la ujazaji maji kwenye Bwawa la JNHPP iliyoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kushuhudiwa na Marais wastaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete, Spika Dk Tulia Ackson na wengine wengi.

Amesema matarajio yao ni baada ya mradi huo kukamilika utapunguza makali ya bei ya ununuzi wa umeme, lakini pia utakuwa bora na salama.

“Hiki ambacho kinafanyika leo hapa ni cha kupongezwa sana, kwani Ilani ya CCM inatekelezwa, tumpongeze Rais Samia kwa uthubutu huo,” amesema.

Kinana amesema katika kuhakikisha wanazungumzia mradi huo kwa kina wanatarajia kufanya ziara ya kichama katika mradi huo.

Amesema chama kipo pamoja na Rais Samia katika kutekeleza miradi mbalimbali nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!