May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kinana: Waliotajwa ripoti ya CAG wawajibishwe

Makamu Mwenyekiti wa chama tawala Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana

Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa chama tawala Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameishauri Serikali inayoongozwa na chama hicho kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wale waliyotajwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Kinana ametoa ushauri huo leo Jumatano tarehe 27 Aprili 2022 ikiwa ni siku ya nne nay a mwisho ya ziara katika mikoa minne akianzia Pwani, Tanga, Kilimanjaro na kumalizia Arusha.

Ushauri huo kwa Serikali anaitoa kipindi ambacho Ripoti ya CAG Charles Kichere inayoishia 30 Juni 2021 iliyowasilishwa bungeni na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni, imeonesha wizi na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma.

Akizungumza kwenye mkutano wa ndani wa chama hicho mjini Arusha, Kinana amesema ni muhimu wote waliyotajwa kwenye ripoti ya CAG kuchukuliwa hatua.

“Wakati umefika kwa serikali kuchukua hatua kwa wahusika waliyotajwa. Ripoti ile inaonesha mambo ya hovyo. Si uzushi imefanywa kisayansi na kitaaluma imeandikwa,” amesema Kinana.

“Mimi nadhani ingekuwa vyema hatua ziwe zinachukuliwa papo kwa papo ili watu waogope kutumia fedha za umma,” amesema Kina a huku akishangliwa na wanachama wa chama hicho.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Charles Kichere

Kinana ambaye alikuwa anahitimisha ziara yake ya mikoa minne kukagua uhai wa chama, amesema pamoja na kwamba hana mamlaka ya kutoa amri kwa serikali lakini atamwambia Rais Samia juu ya ushauri huo.

“Kwa nafasi yangu nazungumza kwa niaba ya mwenyekiti wetu ambaye ni Rais kwamba wahusika wachukuliwe hatua,” amesema.

Kinana aliyewahi kuwa katibu mkuu wa CCM amesema lazima kuwe na utaratibu wa kuwajibika mtu anapofanya kosa.

“Tujenge utamaduni wa kuwahi bila mtu akae pembeni apishe wengine. Kwani si kuna wengi wana uwezo hawana kazi! wakae pembeni waje wengine” amesema

“Kila ripoti ya CAG inapotolewa tukianzia na hii wale wanaotajwa wawajibike. Vyombo vya serikali vichukue hatua kwa yale yaliyotajwa mle ili fedha za wananchi zisichezewe,” amesema.

error: Content is protected !!