January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kinana azidi kuinanga CCM, adai wanatumia `mabavu`

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema kuwa ndani ya chama hicho, wamejaa watu wanaotumia vibaya madaraka yao na wanaofuja fedha za umma kwa masrahi yao binafsi. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Amesema hakuna la kupinga kuwa ndani ya serikali ya CCM hawapo watu wanaotumia vibaya madaraka yao na wanatumia vibaya fedha za umma kwamba wapo wengi wasiokuwa waaminifu wanaokula fedha za umma.

Kinana alitoa kauli hiyo juzi wakati wa mkutano wa hadhara uliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mirongo mjini hapa, ambako kulihudhuliwa na wanachama na wafuasi `kiduchu` wa chama hicho.

Amesema kuwa ndani ya CCM kuna makosa mengi yaliyofanyika na kwamba hakuna mtu atakayepinga suala hilo kwani kuna mapungufu mengi yanayohitajika kufanyiwa marekebisho ili watanzania waendelea kukiamini chama hicho.

“CCM tumefanya makosa mengi, sikatai kama hatujafanya makosa, kuna makosa madogo madogo ambayo yanahitajika kurekebishwa na yapo mazuri mengi yaliyofanywa na chama chetu.

“Tunafahamu kuna kasoro zipo na kuna watu wabaya ambao wanakula hela za Wananchi ndani ya CCM wapo na maofisini wanaoiba hela za walipa kodi wamejaa, watu hawa tutashughulika nao taratibu,” amesema Kinana.

Hata hivyo katika kile kilichoonekana Kinana kutaka kuweka wazi kwamba marais waliotangulia hawakuwa na uwezo wa kuongoza taifa ni pale alipowaomba watanzania kumchagua mgombea Urais wa CCM, John Magufuli, kwamba ndiye mwenye uwezo wa kubadilisha mfumo kandamizi uliyopo.

Amesema kuwa Magufuli ndiye mwenye uwezo wa kuibadilisha CCM na kuondoa mfumo `mchafu` yaliyopo, akitolea mfano wa utoaji wa ajira kwa bahasha ambao unasababisha watoto wa maskini kukosa ajira.

Wakati baadhi ya makatibu wa mikoa na wilaya wa chama hicho wakipinga utaratibu wa kusomba watu kwenda kwenye mikutano, juzi hali hiyo iliendelea ya kuchukua wafuasi kutoka mikoa jirani na wilayani.

Hata hivyo wakati mkutano huo unafungwa saa 11:30 jioni, kabla ya saa 12:00, mshereheshaji aliyekuwa akiongoza mkutano huo, alisikika akisema: “Jamani wale wanachama wa Bugogwa, katibu wenu yupo hapa anawasubiri kwa ajili ya safari,” amesema Mshereheshaji.

error: Content is protected !!