August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kinana awapigia debe wanawake, vijana uchaguzi CCM

Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, ametaka wanachama wanawake wapewe kipaumbele katika chaguzi za nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho, huku akiwahamasisha vijana kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Rukwa … (endelea).

Kinana ametoa wito huo leo Jumanne, tarehe 26 Julai 2022, akizungumza na wanachama wa CCM Mkoa wa Rukwa.

Ameshauri wagombea wanawake wapewe kipaumbele kwenye chaguzi hizo, kwani ni waaminifu, wanatenda haki na hawapendi dhuluma.

“Wanawake wamegombea wengi, hakikisheni mnawapitisha hawa kina mama. Wakina mama ni zaidi ya nusu ya Watanzania, wakigombea nafasi lazima muwape kipaumbele kwa sababu ni waaminifu, wa kweli, watenda haki. Wakina mama hawapenda dhuLuma na ni walezi wazuri wa familia,” amesema Kinana.

error: Content is protected !!