MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka madiwani na wabunge kukataa kupitisha miswada ya sheria yenye kukandamiza haki na kuminya fursa ya wananchi wanyonge kujiendeleza kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Korogwe … (endelea).
Pia, amesema sasa ni wakati muafaka kulitazama vyema kundi la wajasiriamali wadogo wakiwemo mamalishe na bodaboda ili wawekewe mazingira mazuri ya kunufaika na juhudi zao.
Kinana ameyasema hayo leo Jumatatu, tarehe 25 Aprili 2022 mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga wakati akizungumza na wana CCM katika ukumbi wa Lembeni, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kujitambulisha kwa wanachama.
“Madiwani nyinyi ndio mnaosimamia sheria za Halmashauri, mkiona sheria hazina uhusiano na wananchi kataeni. Mkiletewa sheria pelekeni kwa wananchi waulizeni, rahisisheni maisha ya watu muwasidie wakue,” amesema na kuongeza:
“Wabunge wa Bungee la Jamhuri ya Muungano…sheria ikija bungeni waambieni (serikali) kwa sasa hatuipitishi mpaka tukashauriane na wananchi,” alisema.
Kinana ameanza ziara mikoa ya Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
Leave a comment