Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kina Mdee watinga bungeni, Spika awaruhusu kuuliza maswali
Habari za SiasaTangulizi

Kina Mdee watinga bungeni, Spika awaruhusu kuuliza maswali

Mbunge wa Viti Maalum (asiye na chama), Grace Tendega akiuliza swali bungeni
Spread the love

 

LICHA ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kuyaondoa maombi Halima Mdee na wenzake 18 ya kuomba kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema, wabunge hao wa viti maalum wameendelea kuhudhuria vikao vya Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Maombi hayo ya kina Mdee, yaliondolewa mahakakani hapo jana Jumatano, tarehe 22 Juni 2022 na Jaji John Mgetta kutokana na kasoro zilizobainika katika jina la mujibu maa kwaonza ambaye ni Chadema.

Jaji Mgetta alisema, Mdee na wenzake walipaswa kufungua maombi hayo kwa kutaja jina sahihi la bodi hiyo kwa mujibu wa sheria ambapo walitakiwa kuandika “Registered Body of Trustees” badala ya Body of Trusties, waliyoandika.

Kwa uamuzi huo wa Mahakama na Katiba ya Tanzania, Mdee na wenzake 18 walioapishwa tarehe 24 Novemba mwaka 2020 kuwa wabunge wa viti maalum walipoteza sifa za kuwa wabunge wa Bunge kwani ili uwe mbunge lazima uwe na chama na wao kwa sasa hawana chama cha siasa.

Hata hivyo, leo Alhamisi tarehe 23 Juni 2022, baadhi yao wamehudhuria kikao cha 50 kinachoongozwa na Spika wa Bunge hilo, Dk. Tulia Ackon na kuwapa fursa ya kuuliza maswali ya nyongeza.

Baadhi ya wabunge hao waliopewa fursa ya kuuliza maswali ni, Tunza Malapo, Salome Makamba, Kunti Majala na Felister Njau. Aidha baadhi waliohudhuria ni Sophia Mwakagenda, Naghenjwa Kaboyoka na Conchesta Rwamlaza.

Wengine kwenye kundi hilo la wabunge 18 ni, Esther Matiko na Ester Bulaya; Nusrat Hanje; Jesca David Kishoa; Cecilia Pareso, Agnesta Lambart, Asia Mohammed, , Stella Flao, Anatropia Theonest, na

Mdee na wenzake walifungua maombi mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema, jambo ambalo lilikuwa linawafanya kupoteza sifa za kuendelea kuwa wabunge.

Walifikia uamuzi wa kukimbilia mahakamani, baada ya Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, kuamua tarehe 27 Novemba 2020, kuwavua uanachama na baadaye mkutano wa Baraza Kuu wa 11 Mei 2022, kusikiliza rufaa zao na kufikia uamuzi wa kuwatimua.

Mbunge wa Viti Maalum (asiye na chama), Salome Makamba akiuliza swali bungeni

Chadema walifikia uamuzi wa kumtimua Mdee na wenzake, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), kufuatia kupatikana na makosa ya usaliti, kughushi nyaraka za chama na kisha kujipeleka bungeni kujiapisha kuwa wabunge, kinyume na maelekezo ya chama chenyewe.

Wote kwa pamoja, waliapishwa kuwa wabunge, tarehe 24 Novemba 2020 na aliyekuwa spika wa wakati huo, Job Ndugai.

Mara baada ya Baraza Kuu kubariki uamuzi wa kuwavua uanachama wanachama hao, wote kwa pamoja walifungua shauri mahakamani, ambapo pamoja na mambo mengine, waliomba kuruhusiwa kufungua kesi ya msingi na kutoondolewa bungeni, hadi kesi yao ya msingi itakapomalizika

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!