Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kina Mdee waendelea kutinga bungeni, wauliza maswali
Habari za SiasaTangulizi

Kina Mdee waendelea kutinga bungeni, wauliza maswali

Sophia Mwakagenda
Spread the love

 

SIKU mbili kupita tangu Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kuyaondoa maombi Halima Mdee na wenzake 18 ya kuomba kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema, baadhi yao wameendelea kuhudhuria vikao vya Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Maombi hayo ya kina Mdee, yaliondolewa mahakakani hapo juzi Jumatano, tarehe 22 Juni 2022 na Jaji John Mgetta kutokana na kasoro zilizobainika katika jina la mujibu maa kwaonza ambaye ni Chadema.

Jaji Mgetta alisema, Mdee na wenzake walipaswa kufungua maombi hayo kwa kutaja jina sahihi la bodi hiyo kwa mujibu wa sheria ambapo walitakiwa kuandika “Registered Body of Trustees” badala ya Body of Trusties, waliyoandika.

Kwa uamuzi huo wa Mahakama na Katiba ya Tanzania, Mdee na wenzake 18 walioapishwa tarehe 24 Novemba mwaka 2020 kuwa wabunge wa viti maalum walipoteza sifa za kuwa wabunge wa Bunge kwani ili uwe mbunge lazima uwe na chama na wao kwa sasa hawana chama cha siasa.

Hata hivyo, leo Ijumaa tarehe 23 Juni 2022, ikiwa ni siku ya pili baadhi yao wamehudhuria kikao cha 51 kinachoongozwa na Naibu Spika wa Bunge hilo, Mussa Zungu na kumpa nafasi Sophia Mwakagenda kuuliza swali la nyongeza.

Aidha, jana Alhamisi baadhi yao kwenye kundi hilo la Mdee na wenzake 18 walitinga bungeni kama kawaida na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackon kuwapa fursa ya kuuliza maswali pamoja na kuchangia bajeti ya serikali kwa mwaka 2022/23.

Jana Alhamisi, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu alisema baada ya uamuzi wa mahakama walimwandikia barua Spika wa Bunge kupitia barua pepe ya katibu wa Bunge kumjulisha uamuzi wa Mahakama pamoja na kuambatanisha hukumu yenyewe.

“Sisi kwa upande wetu, wajibu wetu ni kuhakikisha taarifa ya hukumu inafika kwa Spika na tayari tumefanya hivyo kwa kumwandikia barua jana jioni (juzi) na tumeituma kwa barua pepe inatotumika anayoitumia katibu wa Bunge,” alisema Mwalimu na kuongeza:

“Tumemwomba Spika atekeleze barua ya Chadema ya Mei 12 mwaka huu ya baraza kuu kuridhia kuwavua uanachama Mdee na wenzake tuliyomtumia nay eye kipindi kile akasema kuna jambo mahakamana anasubiri na sisi tumemkumbushia kuna uamuzi huu wa mahakama na tumeambatanisha hukumu kwa ajili ya utekelezaji wake.”

Mwalimu aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema alisema barua hiyo ni ya kumbukumbu C/HQ/ABM/PARL/33/38 ya Juni 22 mwaka huu iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na nakala imetumwa kwa msajili wa vyama vya siasa na mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), “kwa hiyo sisi tumetimiza jukumu letu.”

Dk. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania

Jitihada za MwanaHALISI Online kumpata Spika wa Bunge, Dk. Tulia ama Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi kujua kinachoendelea kuhusu suala hilo hazijafanikiwa.

Mdee na wenzake walifungua maombi mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema, jambo ambalo lilikuwa linawafanya kupoteza sifa za kuendelea kuwa wabunge.

Walifikia uamuzi wa kukimbilia mahakamani, baada ya Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, kuamua tarehe 27 Novemba 2020, kuwavua uanachama na baadaye mkutano wa Baraza Kuu wa 11 Mei 2022, kusikiliza rufaa zao na kufikia uamuzi wa kuwatimua.

Mbali na Mdee, wengine waliofukuzwa Chadema, ni waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu (CC), Esther Matiko na Ester Bulaya; aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Bawacha (Bara), Hawa Subira Mwaifunga na aliyekuwa katibu mkuu wa Bawacha, Grace Tendega.

Wengine, ni aliyekuwa Katibu mkuu wa Baraza la Vijana la chama hicho (BAVICHA), Nusrat Hanje; aliyekuwa Naibu katibu mkuu wa Bawacha (Bara), Jesca David Kishoa; Cecilia Pareso, Agnesta Lambart, ambaye alikuwa mwenezi wa Bawacha na Tunza Malapa, aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema, mkoani Mtwara.

Katika orodha hiyo, wamo pia Asia Mohammed, aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa Bawacha (Zanzibar), Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Flao, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!