Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kina Mbowe wapewa ‘diary’ ya shahidi, kesi yaendelea
Habari za SiasaTangulizi

Kina Mbowe wapewa ‘diary’ ya shahidi, kesi yaendelea

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na wenzake wakiwa mahakamani
Spread the love

 

UPANDE wa utetezi, katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, umepewa ‘diary’ aliyokutwa nayo kizimbani shahidi wa pili wa jamhuri, Ricardo Msemwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Diary hiyo, alikutwa nayo Ijumaa iliyopita tarehe 12 Novemba 2021, wakati akitoa ushahidi wake kwenye kesi ndogo ya kupinga maelezo ya onyo wa mshtakiwa, Mohamed Ling’wenya yasipokelewe mahakamani hapo,

Wakidai, mtuhumiwa huyo hakuandikwa maelezo katika kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, tarehe 7 Agosti 2020 bali alisainishwa karatasi yenye maelezo yaliyodaiwa kuwa ya kwake katika Kituo cha Polisi cha Mbweni jijini humo.

Upande wa utetezi unaowatetea Mbowe, Ling’wenya na Halfan Hassan Bwire, Adam Kasekwa waliweka pingamizi la kumkataa shahidi huyo kwamba amekosa sifa.

Hata hivyo, pingamizi hilo limetupiliwa mbali leo Jumatano, tarehe 17 Novemba 2021 na mahakama hiyo, mbele ya Jaji Joachim Tiganga anayeisikiliza kesi hiyo huku akiagiza mawakili wa pande zote kwenda kuikagua kuona imeandikwa nini.

Jaji Tiganga aliahirisha kwa dakika 20 ili kutoa fursa ya diary hiyo kukaguliwa na mara baada ya mahakama kurejea, mawakili wa pande zote walitambulisha pande zao huku Jeremiah Mtobesya aliyewakilisha upande wa utetezi akitaka kuzungumza jambo na kuibua mvutano mdogo.

Ilikuwa hivi;

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji, muda mfupi uliopita tumetoka kwenye zoezi la kukagua diary.

Wakili wa Serikali: Robert Kidando-Objection Mheshimiwa Jaji. Hilo haliruhusiwi hata kidogo na hatuko tayari kuona anaendelea. Uamuzi mdogo umeshatolewa.

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji, sijui niongee nini nisionekane namkosea heshima kaka yangu.  Kwamba sisi hatukuwa tumeenda kufanya mchezo wa kitoto na kisha kurejea nyumbani.

Jaji: Nini hasa ulitaka?

Mtobesya: Nilikuwa nataka kuipeleka Mahakama chini ya kifungu cha 176 (1) chini ya Sheria ya Ushahidi. Mahakama ikiona inafaa imtake atoe nakala ya nyaraka yake.

Jaji: Sasa mimi sijajua nyie mmeona nini. Labda tuingie ofisini tukaone mmeona nini. Unasemaje Mr Robert Kidando?

Wakili wa Serikali: Sawa Mheshimiwa Jaji.

Jaji: Naahirisha kwa muda.

Baada ya muda, Jaji Tiganga alirejea na kesi ikatajwa na mawakili wa pande zote kwa maana ya Chavula ametambulisha mawakili wa mashtaka na Peter Kibatala akitambulisha mawakili wa utetezi kisha Mtobesya akasimama.

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji, wakati umetupatia nafasi ya kwenda kukagua diary, tumekuta kuna mambo yapo relevant na kesi yetu. Kwa sababu hiyo, kupitia kifungu 176 (1) ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019, tunaiomba Mahakama tupatiwe kama kielelezo.

Jaji: Upande wa mashitaka?

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi.

Jaji: Basi hiyo relevant part Mahakama inaelekeza ichukuliwe na iingie kama sehemu ya kielelezo.

Shahidi anaendelea kutoa ushahidi wake mahakamani hapo. Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

1 Comment

  • Lugha unayoitumia hasa kwenye vichwa vya habari ina ujakasi. Unatiliwa mashaka kuwa unatumija ndivyo sivyo kinyume na wajibu wako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!