January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kina Mbowe wakataa taarifa za tigo

Spread the love

 

MAWAKILI wa utetezi, katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wamekataa shahidi wa Jamhuri, Meneja wa Kitengo cha Sheria cha Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania PLC, Gladys Fimbari, kuitambua namba ya mtandao wa Tigo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mawakili hao wamechukua hatua hiyo leo Alhamisi, tarehe 13 Januari 2022, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu, iliyopo Mawasiliano jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janetreza Kitali, kumtaka Fimbari kuitambua namba 0780900174, kuwa ya mtandao gani, ambapo alijibu akidai ni ya mtandao wa Tigo. Kwa mujibu wa usajili, imesajiliwa jina la Tigo Pesa Tigo Pesa

Baada ya kutoa majibu hayo, Wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya alipinga jibu hilo, akidai shahidi huyo hakuzungumzia mtandao huo wakati anatoa ushahidi wake.

Namba hiyo inadaiwa kutuma Sh.500,000 kwenda kwenye namba 0787555200, inayodaiwa kuwa ya Dennis Leo Urio.

Majibizano yao yalikuwa kama ifuatavyo;

Mtobesya: Obejection, mtu wa Tigo alishakuja na yeye sio mtu wa Tigo, ataitambuaje kama ya Tigo?

Tunasisitiza aishie hapo, hiyo namba aitaje irekodiwe. Asiitaje ya kampuni gani. Hii ni document labda watuambie kuna sehemu pembeni imeonesha Tigo.

Jaji: Nafikri hiyo ndio kimsingi kazi ya wakili wa utetezi, unapohitaji kui-auestion document yenyewe ni wakati wa cross examination. Kama document imeingia mahakakani unamwambia shahidi baadhi ya vitu huwezi kuzungumza na vingine kuzungumza, nafikiri utakuwa unakwenda mbali zaidi.

Mtobesya: Akiwa anasoma maana yake atakuwa anarekebisha, anaposema namba ya Tigo haipo hapa, anaongezea ndiyo manaa tunasema she is doing over. Na kusema mtatumia cross examination hata kama tuki-cross examination is arleady there na mtu mwingine akiikuta hawezi kujua tulisimama kuipinga.

Jaji: Namba ya Tigo tuiondoe?

Mtobesya: Correct

Baada ya maelezo hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi wa Serikali, Abdallah Chavula, alijibu “kwa maslahi ya muda na maslahi ya haki, sie hilo swali tunaachana nalo hatutaendelea na swali.”

Shahidi huyo wa jamhuri anaendelea kutoa ushahidi wake, baada ya kuwasilisha mahakamani hapo taarifa za usajili na miamala ya fedha ya namba za simu za 0782237913, 0787555200 na 0784779944.

Inayodaiwa kufanyika kati ya tarehe 1 Juni hadi 31 Julai 2020, zilizoombwa na Kitengo cha Uchunguzi wa Kisayansi cha Jeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa ushahidi wa Fimbari, namba 0784779944, inadaiwa kumilikiwa na Freeman Aikael Mbowe, 0787555200 ni ya Denis Urio na 0782237913 inamilikiwa na Halfan Bwire Hassan, hata hivyo namba hiyo inayodaiwa kuwa ya Hassan, imesajiliwa kwa jina la Gadson Mmuru.

Katika kesi hiyo yenye mashtaka sita ya ugaidi, Mbowe anadaiwa kutoa fedha zaidi ya Sh.600,000 kwa ajili ya kufadhili vitendo vya ugaidi.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo yenye mashtaka sita ya ugaidi ni waliokuwa makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Halfan Bwire Hassan, Mohammed Ling’wenya na Adam Kasekwa.

error: Content is protected !!