Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Michezo Kimwanga CUP yazidi kutimua vumbi
Michezo

Kimwanga CUP yazidi kutimua vumbi

Spread the love

MASHINDANO ya mpira wa miguu ya Kimwanga CUP ya kuwania ng’ombe yanazidi kutimua vumbi huku timu kadhaa zikiendelea kumenyana katika hatua ya makundi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Katika mchenzo uliochezwa leo tarehe 1 Machi 2023, ulizikutanisha timu mahasimu wa jadi  za Kamongo na Darton zimeshindwa kupata mbabe baada ya kutoka suluhu ya kutofungana kwenye mchezo uliopepetwa katika Uwanja wa Bubu Kata ya Makurumla Manispaa ya Ubungo.

Katika mchezo huo uliokusanya mashabiki lukuki kwa kila timu, ambapo timu hizo zilishindw kupata mbabe katika dakika 90 za mchezo huo.

Mchezo huo ambao mwamuzi wa kati alikuwa Hamis Pondamali akisaidiwa na waamuzi wa pembeni ambao mara zote walikuwa na kibarua cha kufuatilia hatua zote muhimu katika mchezo huo.

Akizungumza mmoja wa mashabiki wa mpira wa miguu ambaye alihudhuria uwanjani hapo, Saidi Mjeshi amesema kwa muda wa zaidi ya miaka 10 timu za mpira wa miguu pamoja na mashabiki walikosa burudani ya soka na sasa wanaona mwanga mpya.

Diwani wa Kata ya Makurumla, Bakari Kimwanga (aliyesimama) akiwatambulisha wanahabari za michezo nchini Jimmy Chika ( kulia), Juma Kasesa (katikati) kwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Kimwanga CUP, Issa Salumu ( kushoto).

“Huyu diwani (Bakari Kimwanga) amefanya jambo kubwa kwanza Serikali ya mama Samia inataka michezo na yeye ameileta kwa kweli sasa tuna uhalika wa kupata burudani kila siku jioni hapa Uwanjani kwetu kwa Bubu.

“Lakini tu kinachovutia ni zawadi iliyoandaliwa na diwani kwa mshindi wa kwanza ya ng’ombe na sasa tunashuhidia kila timu ikihangaika kujiweka sawa ili mradi ijikusanyie alama tatu muhimu katika kila mchenzo.” amesema Mjeshi

Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Diwani wa Kata ya Makurumla, Bakari Kimwanga ambaye ndiye aliandaa mashindano hayo, amesema kuwa amedhamiria kukuza vipa ji kupitia mpira wa miguu.

” Kwetu tunaendelea kutoa nafasi za taasisi mbalimbali ambazo zinataka kuja kudhamini mashindano yetu lengo likiwa ni kuwa na mashindano yaliyo bora na ya mfano.

“Kubwa tunashuhudia idadi kubwa ya mashabiki kila siku tunaona uwanja unakusanya zaidi ya watu 1500 hadi 2000 ambao wanakuja kupata burudani.


“Milango yetu ipo wazi kwa mtu au taasisi yoyote inayotaka kuja kudhamini mashindano haya ya Kimwanga CUP ikiwamo kuboresha zawadi kwa washindi.

“Tunataka kuonyesha burudani hasa kwa jamii yetu,” amesema Kimwanga

1 Comment

  • @THINK/Dedication/Remember”@ EMPLOY/US THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 32.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!