August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kimenuka Yanga, wachezaji wagomea mazoezi

Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini

Spread the love

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida jana asubuhi katika uwanja wa Uhuru, baada ya wachezaji wa klabu ya Yanga kugomea mazoezi yaliyokuwa yanasimamiwa na kocha wao Mkuu, George Lwandamina baada ya kinachosemekana kuwa wachezaji wanadai mshahara ya mwezi Novemba.

Baada ya hali hiyo kutokea kocha Lwandamina akishirikiana na viongozi wengine wa benchi la ufundi walijaribu kila jitihada ili kuwashawishi wachezaji kuendelea na mazoezi lakini ilishindikana na kuendelea kubaki na msimamo wao.

Katika kudhibitisha juu ya madai ya mishahara kwa wachezaji ndani ya klabu hiyo, Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Baraka Deusdedit amesema hali hiyo imetokea baada ya uongozi kubadilisha utaratibu wa kutoa mishahara tofauti na walivyokuwa wanalipa hapo awali.

“Sio mgomo wala jambo kubwa kama watu wanavyolichukulia ni kubadilika tu kwa utaratibu wa kulipa mishahara tofauti na hapo awali maana mwenyekiti alishawazoesha kuwapa mshahara mwanzo wa mwezi na sio mwisho wa mwezi,” amesema Baraka.

Aidha aliongezea ya kuwa mpaka sasa uongozi unalishughulikia suala hili na mpaka kufikia jioni au kesho wachezaji wanaweza kurejea mazoezini na kujiandaa na mchezo unaofuata wa ligi siku ya Ijumaa dhidi ya African Lyon.

“Nafikili ni suala linalofuatiliwa kiuongozi na litakaa vizuri tu na wachezaji wataweza kurejea mazoezini muda wowote”

Licha ya kubadilika kwa utaratibu wa kulipa mishahara kama ilivyosemwa na uongozi wa klabu hiyo, pengine hali mbaya ya kiuchumi imeikumba klabu hiyo ndio inayosababisha hali hiyo kutokea kutokana na kutegemea fedha kutoka mfukoni kwa mtu ili kulipa mishahara na sio vyanzo vya mapato vya klabu hiyo.

error: Content is protected !!