JESHI la Polisi nchini limesema tayari uchunguzi umeanza dhidi ya picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii huku zikimuonesha askari wa usalama barabarani (trafki) akiwa ameshika fedha mkononi.
Picha nyingine zilionesha fedha zikiwa ndani ya gari kwenye kiti huku picha hizo ziiambatana na ujumbe unaosema “ askari akamatwa akiwa na pesa za rushwa”. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Januari, 2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP- David Misime imesema picha hizo zilivyoanza kusambaa hatua zilianza kuchukuliwa kwa kushirikiana na wadau wengine.
Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa hakuna aliyepo juu ya sheria hivyo hatua kali na stahiki kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na ushahidi utakaopatikana zitachukuliwa.
Aidha, taarifa za awali zinadai kuwa Askari huyo wa usalama barabarani wa Mkoa wa Iringa, anadaiwa kukamatwa na fedha anazodaiwa kuzikusanya kama zao la rushwa kutoka kwa madereva na wamiliki wa magari Januari 18, 2022.
Picha za tukio hilo zilionyesha ndani ya gari kukiwa na noti za Sh1,000, Sh2,000, Sh5,000 na Sh10,000 zilizokunjwa na nyingine askari mmoja akiwa amezishika baada ya kuzipanga.
Leave a comment