Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kimenuka Bodi ya Korosho
Habari za Siasa

Kimenuka Bodi ya Korosho

Zao la Korosho
Spread the love

TUME ya watu watano, imeundwa ili kuhakiki korosho yote iliyopokelewa, iliyouzwa na fedha zilizopatikana baada ya kuwepo kwa matumizi ya fujo ya Sh. 52.2 Bil. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Pia, tume hiyo itaihakikisha serikali, kwamba wote waliolipwa fedha hizo ni wakulima waliostahili kulipwa.

“Tuhakiki majina yaliyotoka kwenye vyama vya msingi kuja vyama vikuu, na yaliyokwenda kwenye mfumo wa malipo kwenye Benki ya TIB kwa kushirikiana na Bodi ya Mazao mchanganyiko,” alieleza Japhet Hasunga, Waziri wa Kilimo.

Hasunga mbele ya vyombo vya habari jijini Dodoma, juu ya ufisadi wa kutisha uliofanywa na Dodi ya Korosho pamoja na vyama vya msingi vya ushirika amesema, bodi hiyo imefanya ufisadi wa kutisha kwa kujinufaisha katika kutumia vibaya kiasi hicho cha fedha.

Amesema, fedha hizo (Sh. 5202 bilioni) zilizokuwa katika Mfuko wa Wakfu wa kuendeleza zao la Korosho, baada ya serikali kutangaza kufuta mfuko huo Desemba 2016.

Fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya mambo makubwa mawili, ambayo ni kujenga viwanda vitatu vya kubangua korosho na maghala katika maeneo ya Mkinga – Tanga, Tunduru – Ruvuma na Mkuranga – Pwani.

Hasunga amesema, kazi ya pili ya fedha hizo ilikuwa ni kwa ajili ya kuendeleza zao la korosho ili kuhakikisha mikoa ambayo inazalisha zao hilo inaongeza uzalishaji.

“Nini kimejitokeza, kilichojitokeza wakati hizo fedha zilizobaki wakati bodi yetu ya korosho badala ya kutekeleza hayo maagizo ya serikali, waliamua kukiuka maagizo wakabadilisha matumizi.

“Viwanda havikujengwa, maghala hayakujengwa wakatumia fedha hizo tofauti na maagizo ya serikali. Kilichotushtua mwaka huu wakati minada inaendelea, wale walioagiza magunia kwa misimu iliyopita, wameleta madeni kwamba wanaidai serikali magunia yaliyopita,” amesema Asunga.

Amesema, kampuni moja inadai bilioni 7 na nyingine bilioni 5 ambapo alidai, zaidi ya bilioni 13 zinadaiwa ambapo madai yao ni kwamba walisambaza magunia miaka 2017-2018.

“Na wakati huo utaratibu uliokuwepo, mnunuzi alikuwa akinunua analipia magunia, sasa swali hizo fedha zilizokusanywa za magunia ni kwanini hazijalipwa na kwanini madeni hayo yaje leo?

“Tulipoomba maelezo kutoka bodi, tulitaka kujua matumizi ya fedha bilioni 53.2 yalitumikaje, wao wanasema zile fedha walitumia bilioni 28.1 kununua viuatilifu, lakini kibaya zaidi wanasema wametumia zaidi ya bilioni 12 kulipia magunia ambayo yaliyonunuliwa,” amesema.

Amesema, fedha zilizopangwa kwa ajaili ya viwanda, nazo zilibadilishwa matumizi huku maelezo yaliyotolewa yakiwa hayajitoshelezi.

“Fedha zilizobaki kwa ajili ya viwanda, fedha hizo walichukua wakalipa vyama vikuu vya ushirika eti vilienda kulipia madeni ya benki kinyume na maelekezo ya Serikali.

“Mfano Chama Kikuu cha Tanecu kilipewa zaidi ya bilioni 1.8 kulipia deni na Chama cha Koreku kilipewa bilioni 2.2, kibaya zaidi wanasema, wakati wanasimamia hilo zoezi, walilipana milioni 638.9 watendaji wa bodi,” amesema na kuongeza;

“Fedha zingine wanasema, wamezitumia katika kualika vikao vya wadau na wakatumia fedha kibao zinakaribia bilioni moja kwa ajili ya kuandaa vikao vya wadau.”

Waziri huyo amesema, kutokana na sintofahamu ya fedha nyingi, serikali imeamua kupitia upya mapato na matumizi ya fedha hizo ili kubaini wapi zilipoponyoka.

“Hivyo tumeamua ili tujiridhishe kwanza fedha zilizobaki zilienda wapi, lakini tujiridhishe matumizi yake na tuone kama kuna vibali vilitolewa na ni nani katoa hivyo vibali.

“Tumeamua kumwagiza CAG (Mkaguzi Mkuu wa Serikali) aende ahakiki fedha hizo, akishahakiki atuletee taarifa ili serikali ichukue hatua zinazostahili. Inatisha na inatutisha vibaya hata yale malipo lazima tuhakiki vizuri, kwani kuna kichaka watu wanakitumia kinyume na taratibu tumesema tutapambana na rushwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!