March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kimbunga Maria chapiga hodi Marekani

Spread the love

KIMBUNGA cha Maria kimekivuruga kisiwa cha Puerto  Rico nchini Marekani na kusababisha umeme kukatika katika eneo lote katika kisiwa hicho, anaandika Mwandishi wetu.

Huu ni mfululizo wa Vimbunga katika nchi hiyo kubwa na yenye nguvu kiuchumi duniani.
Kimbunga Maria kimekata umeme katika kisiwa chote cha Puerto Rico, chenye watu milioni 3.5.

Abner Gómez, ambaye ni mkuu wa utoaji huduma za dharura amesema  kuwa watu wote wanaotumia umeme wamekosa huduma hiyo.

Kituo cha vimbunga cha Marekani kinasema kuwa mafuriko makubwa yanaikumba nchi hyo.
Kwa sasa Kimbunga Maria kwa sasa kinaondoka eneo hilo  na kumepunguza nguvu zake hadi kiwango cha pili.

Baada ya kimbunga Maria kuipiga Puerto Rico, gavana ameamrisha watu kusalia nyumbani kuanzia saa 12 jioni hadi asubuhi.

Hii ni hatua ya kwanza ya kuwazuia watu kusalia nyumbani ili kuwaepusha na ajali kutokana na nyaya za umeme zilizoanguka.

error: Content is protected !!