April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kimbunga Keneth chauwa watatu

Spread the love

KIMBUNGA Keneth kimesababisha vifo vya watu watatu katika visiwa vya Comoro. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti kwamba kimbunga hicho kilichoambatana na upepo mkali wa kasi ya kilomita 220 kwa saa, kilikumba visiwa hivyo  na kusababisha vifo hivyo.

Mamlaka mbalimbali za hali ya hewa ikiwemo Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) ilitabiri kwamba Kimbunga Kenneth kitafika katika nchi za Malawi, Msumbiji na Kusini mwa Tanzania kuanzia jana Alhamisi.

Kwa upande wa Msumbiji, mamlaka nchini humo ililazimika kuhamisha wananchi takribani 30,000  kutoka katika maeneo yaliyotabiriwa kupitiwa na Kimbunga Keneth na kupelekwa katika sehemu salama.

Nchini Msumbiji, Kimbunga Keneth kimefanya uharibifu maeneo ya kaskazini mwa taifa hilo. Hata hivyo, taarifa zinaeleza kwamba nchi hiyo huenda ikakumbwa tena na dhoruba nyingine.

Leo tarehe 26 Aprili 2019 kimbunga hicho kimetajwa kupungua kasi yake.

error: Content is protected !!