Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kimbunga ACT-Wazalendo; CCM yaungana na CUF ‘kulaani’
Habari za SiasaTangulizi

Kimbunga ACT-Wazalendo; CCM yaungana na CUF ‘kulaani’

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeungana na Chama cha Wananchi (CUF) kulalamikia hatua ya waliokuwa wanachama wa chama hicho (CUF) kubadili rangi za majengo waliyokuwa wakitumia kupaka rangi ya ACT-Wazalendo. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM akizungumza katika Uzinduzi wa Mkakati Maalum wa CCM wa kukomaza demokrasia nchini uliofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, alilalamikia hatua iliyochukuliwa na ACT-Wazalendo dhidi ya CUF.

Bila kutaja jina la ACT-Wazalendo Dk. Bashiru alisema, hatua ya baadhi ya watu kuchoma benderea pamoja na kupaka rangi majengo ya vyama vingine ni kosa la jinai.

“Kuna watu wanajiita wafuasi wa vyama fulani wameanza kuchoma bendera za vyama vingine, ni kosa tena la jinai, wanaparamia majumba ya vyama vingine na kuyapaka rangi ya vyama vyao, CCM tusifanye hivyo. Lakini pia CCM tuziagize serikali zetu kusimamia sheria,” amesema Dk.  Bashiru na kuongeza;

“Heshima ya alama ya chama chetu na alama za taifa letu ni wajibu wetu sote, lakini sio tu kuheshimu alama za chama chetu bali tu kuheshimu alama za vyama vingine.

“Hatutarajii katika chama mwanachama yoyote wa CCM kuchoma bendera na kubeza alama ya chama chochote sababu vyama vyote vipo kisheria tunatakiwa kuonyesha mfano.”

Dk. Bashiru ametoa mamaliko hayo wakati ambapo ambao CUF inatoa malalamiko kwamba, ACT-Wazalendo imekuwa ikifanya fujo huku ofisi zilizokuwa zikitumiwa na chama hicho zikibadilishwa na kupakwa rangi ya bendera ya ACT-Wazalendo.

Hekaheka ya kuchoma moto bendera, wanachama wa CUF kuhamia ACT-Wazalendo na zilizokuwa ofisi za CUF kupakwa rangi ya ACT-Wazalendo ziliibuka baada ya Maalim Seif kutangaza rasmi kuhamia ACT-Wazalendo tarehe 18 Machi 2019.

Kutokana na kukerwa na matukio ya ACT-Wazalendo, tarehe 21 Machi 2019, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CUF, Mussa Haji Kombo aliitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufuta chama hicho.

Maalim Seif Shariff Hamad, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF alipoulizwa kuhusu umiliki wa majengo ya chama hicho alisema, CUF inamiliki majengo matatu ambayo ni Mtendeni, Kilimahewa yaliopo Zanzibar na Ofisi Kuu iliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam.

“Watu walikuwa wakitoa maeneo ama majengo yao kufanya ofisi za CUF kwa mapenzi yao, sasa kama wameona mapenzi na CUF yamekwisha na sasa wanabadilisha matumizi, hilo siwezi kuwazuia,” alisema Maalim Seif wakati akitambulishwa rasmi kwenye mkutano uliofanyika katika Makao Makuu ya ACT-Wazalendo, Kijitonyama Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!