Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kimbembe CUF, 369 milioni zatoroshwa
Habari za SiasaTangulizi

Kimbembe CUF, 369 milioni zatoroshwa

Julius Mtatiro, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi – CUF
Spread the love

SHILINGI 369.4 milioni mali ya Chama Cha Wananchi (CUF) zinadaiwa kutoroshwa kutoka Hazina ya Serikali Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Alhamis ya tarehe 05 Januari 2017, anaandika Pendo Omary.

Zinadaiwa kuhamishwa kutoka Hazina kwenda ya NMB, tawi la Temeke katika akaunti Na. 2072300456 ambayo inamilikiwa na CUF ngazi ya wilaya.

Julius Mtatiro, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi – CUF amewaambia waandishi wa habari leo asubuhi jijini Dar es Salaam kwamba, “Baada ya Hazina kuhamisha fedha hizo, watia saini wapya wa Akaunti ya CUF katika benki ya NMB Wilaya ya Temeke tarehe 06 Januari 2016, watia saini hao wakiongozwa na Thomas Malima walichota Sh. 69 milioni.

Pia walihamisha Sh. 300 milioni kwenda kwenye akaunti ya mtu binafsi ya NMB yenye Na. 41401600207 inayomilikiwa na mtu aitwaye Mhina Masoud Omary ambaye ni Diwani wa CUF wilayani Handeni.”

Omary ni anatajwa kama mtu wa karibu wa Prof. Ibrahim Lipumba aliye katika mgogoro na chama cha CUF lakini pia diwani huyo ni mmoja kati ya wanachama wanaoshitakiwa na Bodi ya Wadhamini ya chama hicho.

“Jana Jumatatu wakati tunapokea taarifa nzima za yanayoendelea, kulikuwa na hekaheka kubwa ya kuondoa fedha hizo kutoka kwenye akaunti ya diwani huyo. 150 milioni zimechukuliwa kutoka NMB tawi la Magomeni, kisha 149.5 milioni zikachukuliwa kutoka tawi la Kariakoo.

“Wakati Omary anazunguka kwenye matawi haya kutoa fedha hizi jana alipewa ulinzi wa Polisi waliokuwa wamevalia kiraia wakiwa kwenye magari ya CUF na aliambatana na Thomas Malima wakiwa chini ya usimamizi wa watu wengine wawili, ambao ni Mbunge Magdalena Sakaya (Kaliua) na Abdul Kambaya, mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa kambi ya Lipumba,” amesema Mtatiro.

Hata hivyo tarehe 10 Oktoba mwaka jana, Jaji Francis Mutungi Msajili wa Vyama vya Siasa aliwaandikia barua yenye Kumb. Na. HA.322/362/14/17.Prof. Lipumba na Maalim Seif Sharif Hamad Katibu Mkuu wa CUF akiwajulisha kwamba Ofisi yake imesitisha ruzuku ya CUF iliyokuwa ikitolewa kila mwezi.

“Tunajiuliza, kama Hazina inaweza kukubali kutumika katika michezo michafu tena bila woga, kama Benki ya NMB inaweza kabisa kutumika katika uhuni mkubwa wa namna hii tena dhidi ya taasisi kubwa kama CUF, Je mtu mmoja mmoja yuko salama kifedha namna gani?

“Je fedha za umma zina ulinzi wa kutosha kiasi gani hapo Hazina? Na ni nani anayetoa amri fedha za umma zipelekwe kokote kule bila kuzingatia taratibu, kanuni na sheria za nchi? Mtu huyo yuko juu ya sheria?” amehoji Mtatiro.

Ameeleza kuwa Kitendo hicho ni kipimo tosha cha utendaji wa Ikulu, mifumo ya fedha za nchi yetu na utashi wa Rais John Magufuli katika kupambana na vitendo vya rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!