May 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kimbembe CCM, Chadema umeya Kinondoni

Spread the love

MSUGUANO wa kisiasa umeanza kuinyemelea Manispaa ya Kinondoni wakati huu kuelekea uchaguzi wa meya wa manispaa hiyo, anaandika Faki Sosi.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinamtuhumu Aron Kagurumjuli, Mkurugenzi wa Manspaa ya Kinondoni kwamba, anaandaa mazingira ya kukibeba Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tuhuma hizo zinakuja baada ya Kagurumjuli kuwaandikia Chadema kwamba, Manispaa ya Kinondoni haitakuwa na madiwani zaidi ya theluthi moja ya madiwani waliokuwepo awali jambo ambalo wanalipinga.

Boniface Jacob, aliyekuwa Meya wa Kinondoni akizungumza na mtandao huu amedai, anachokifanya na Kagurumjuli ni kinyume na utaratibu na kwamba, anatumika na CCM.

Hatua iliyochukuliwa na Kagurumjuli inadaiwa kulenga kupata idadi kubwa ya madiwani wa CCM ili waweze kushinda kwa kura na hatimaye manispaa hiyo kuongozwa na chama hicho tawala.

“Hata wakifanya mbinu hizo, bado ushindi wa Ukawa upo pale pale” amesema Jacob.

Kwenye barua hiyo Kagurumjuli ameeleza kuwa, kutakuwa na madiwani viti maalumu wanawake wasiopungua theluthi moja ya madiwani wa kugachaguliwa.

Hata hivyo, Henry Kilewo, Katibu Mkuu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam amejibu barua hiyo akipinga barua ya Kagurumjuli.

“Nimemuandika barua kumueleza. Tungekuwa tumemaliza uchaguzi mkuu ningekubaliana na yeye  lakini kwa hali ilivyo sasa hatuwezi kukubaliana naye na kwasababu baraza likiitishwa madiwani hawatakula kiapo tena,” amesema Kilewo.

Kiwelo ameeleza kuwa, anasimamia sheria na kwamba “hafuati matakwa ya mtu. Wao wanapingana na sheria, sielewi presha inatoka wapi? wa kushinda atashinda na wakukosa atakosa,” amesema Kilewo.

 

error: Content is protected !!