July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kimaro: Waumini tukusanyike kuombea amani

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Kariakoo (KKKT), Eliona Kimaro

Spread the love

VIONGOZI mbalimbali wa dini nchini kutoka madhehebu mbalimbali leo, watakusanyika na katika uwanja wa Taifa kuiombea nchi amani kuelekea katika uchaguzi mkuu. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Mkesha huo utafanyika kwa lengo la kuiombea nchi amani ili kusitokea machafuko katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waumini wanaosali katika ‘Morning glory’ kila siku Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Kariakoo (KKKT) Eliona Kimaro aliwaomba waumini hao kujukuika kwa pamoja katika mkesha huo ili kuungana na watanzania wengine kuiombea nchi.

“Tunaelekea katika uchaguzi mkuu hivyo hatuna budi kuiombea nchi amani kuelekea uchaguzi mkuu ili machafuko yasitokea na tuweze kuwapata viongozi makini kwa ustawi wanchi”amesema Mchungaji Kimaro.

Kabla ya Mchungaji Kimaro kufanyika mkesha huo wa kuiombea nchi amani kulitangulia na semina ya siku nne katika usharika huo kuiombea nchi Kimaro.

error: Content is protected !!