May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kim Poulsen kutangaza kikosi cha Stars

Kim Poulsen

Spread the love

 

KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen anatarajia kutangaza kikosi chake kitakachoingia kambini kwa ajili ya maandalizi dhidi ya Guinea Ikweta. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Mchezo huo wa kundi J wa kufuzu kwa michuano ya kombe la mataifa Afrika utapigwa 25 Machi 2021, nchini Guinea.

Mpaka sasa Stars kwenye kundi hilo inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi, nyuma ya Equtorial Guinea kwa pointi mbili ikiwa nafasi ya pili.

Kabla ya kuvaana na timu ya Taifa ya Guinea Ikweta, Taifa Stars itacheza mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars).

Ikumbukwe Kim Poulsen amekuja amechukua nafasi ya Ettienne Ndayilagije ambaye amesitishiwa mkataba wake kutokana na matokeo mabovu kwenye michuano ya CHAN.

error: Content is protected !!