May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kim Poulsen atua Bongo kuchukua mikoba ya Etienne, sababu za kufukuzwa zaelezwa

Etienne Ndayiragije, Kocha wa Taifa Stars

Spread the love

 

INAELEZWA tayari Kim Poulsen kocha raia wa Denmark yupo nchini kwa ajili ya kukaimu kwa muda nafasi ya aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Etienne Ndayilagije ambaye amesitishia mkataba wake na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Anaripoti kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Ndayilagije ambaye alikuwa anakinoa kikosi cha Taifa Stars toka mswaka 2019, mara baada ya kuchukua mikoba kutoka kwa Emmanuel Amunike ambaye aliyetimuliwa kutokana na matokeo mabovu kwenye michuano ya AFCON iliyofanyika Misri.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa tayari Kim Poulsen amefika nchini toka Jumatatu ya tarehe 7 Februari 2021, na atakaimu kama kocha mkuu wa Taifa Stars kwa muda kuelekea kwenye mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Equtorial Guinea utakaopigwa tarehe 22 Machi 2021.

Kim Poulsen

Hapo awali ilielezwa kuwa Poulsen anakuja nchini kwa ajili ya kuwa mshauri mkuu wa soka la vijana kwa timu zote za Taifa lakini kwanza ataanza na kibarua cha kuionoa Taifa Stars katika michezo ya kufuzu.

Aidha taarifa pia za kuaminika ambazo MwanaHALISI Online imezipata kuhusu sababu kubwa ya kumuondoa Etienne Ndayilagije ni kupata mataokeo mabovu kwenye michuano ya kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) iliyomalizika hivi karibuni nchini Cameroon.

Taifa Stars ilishiriki michunao hiyo na kumaliza nafasi ya tatu kwenye Kundi D, ambapo ilikuwa pamoja na timu za Namibia, Guinea na Zambia.

Katika michezo mitatu iliyocheza kwenye michuano hiyo Taifa Stars ilibuka na ushindi kwenye mchezo mmoja mara baada ya kumfunga Namibia na kwenda sare dhidi ya Guinera na mchezo mmoja walifungwa dhidi ya Zambia na hivyo kujikusanyia pointi nne.

error: Content is protected !!