May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kim Poulsen akoshwa na bao la Samatta

Kim Poulsen, kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania

Spread the love

 

KOCHA wa Timiu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Polusen ameonekana kukoshwa na bao la pili kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki, kati ya Taifa Stars dhidi ya Afrika ya Kati liliwekwa kambani na nahodha wa kikosi hiko Mbwana Samatta. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa kirafiki wa kalenda ya Shirikisho la Mpira Duniani ‘FIFA’ ulipigwa jana tarehe 23 Machi 2022, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, majira ya saa 1 usiku.

Kim amesema kuwa kwa muda mrefu hajaona aina ile ya bao likifungwa kwa ustadi mkubwa na jinsi lilivyotengenezwa kwa kupigwa pasi kutokea nyuma.

“Wakati wangu bora kwenye mchezo wa leo ni bao la pili, kwa muda mrefu sijaoana aina hii ya mpira na pasi, kwa kweli ulikuwa wakati mzuri.” Alisema Kim

Bao hilo lilifungwa dakika ya 62 ya mchezo ambapo mashambulizi yalianzia kwa mlinzi wa kati Bakari Mwamnyeto na kupigwa jumla ya pasi nne mpaka kumfikia mfungaji.

Aidha kocha huyo aliendelea kusema kuwa amejivunia nafasi kikosi chake kwa kutengeneza nafasi nyingi kwa aina ya timu ngumu kama Afrika ya kati jambao ambao limetia faraja.

“Tumetengeneza idadi kubwa ya nafasi, tumefunga mabao matatu, ukiangalia kwenye kwenye ushambuliaji ninafuraha kutengeza idadi nyingi za nafasi dhidi ya mpinzani kama Afrika ya kati, ambao ni timu nzuri na ngumu na wanacheza vizuri.” Alisema kocha huyo

Mabao mengine ya Stars kwenye mchezo huo yalipachikwa kambani na Novatus Dismas kwenye dakika ya tisa, huku na bao lengine likifungwa na George Mpole kwenye dakika ya 90+3.

error: Content is protected !!