Spread the love

 

KIONGOZI wa Korea Kaskazini Kim Un ametuma salamu za pongezi kwa Rais VIadimir Putin baada ya kusherekea Siku ya Ushindi ya Urusi jana tarehe 9 Mei 2022 ,akielezea mshikamano thabiti wa nchi yake na Moscow, shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limeripoti.

Kwa mujibu wa taarifa yake iliyotumwa jana Jumatatu tarehe 9 Mei 2022, Kim anasema kuwa ‘’Mshikamano madhubuti wa muda mrefu kwa sababu ya watu wa Urusi kung’oa vitisho vya kisiasa na kijeshi na usaliti wa vikosi vya adui.’’

Kiongozi huyo ameeleza pia imani yake kwamba, uhusiano wa kimkakati na wa jadi wa urafiki kati ya nchi hizo mbili utakuwa kwa kasi.

Hata hivyo hivi karibuni Korea Kaskazini imeangazia uhusiano wake wa karibu na Urusi , na kuunga mkono hadharani Moscow juu ya uvamizi wake nchini Ukraine.

Aidha mwezi Februari ,ililaumu mzozo wa Ukraine juu ya ‘’sera ya kivita ‘’ya Marekani na Magharibi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *