Thursday , 29 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kim Jong-un aitambia Marekani
Kimataifa

Kim Jong-un aitambia Marekani

Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini
Spread the love

Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini  amesema kuwa, vitisho vya hivi karibuni vya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya nchi yake, ni vya kijinga, anaandika Hellen Sisya.

Kiongozi huyo amesema kuwa, vitisho hivyo ni kichekesho na ameonya kwamba, hadi sasa Marekani haijafahamu uwezo na nguvu kubwa ya Korea Kaskazini.

Amesisitiza kuwa , Pyongyang haiogopi Washington na kwamba, hata Maneva ya kijeshi ya Marekani yaliyofanyika hivi karibuni katika eneo la Korea na yale yanayoendelea sasa huko Australia, ni kujaribu tu kuonyesha uwezo wake uliozoeleka.

Eneo la Peninsula ya Korea limekuwa katika hali tete kutokana na siasa za uhasama zinazotekelezwa na Washington kwa kushirikiana na washirika wake kuilenga Korea Kaskazini. Kwa mara kadhaa Pyongyang imekuwa ikisisitiza kuwa, itaendelea kujiimarisha kijeshi madamu Washington itaendeleza vitisho vyake vya kila uchao dhidi yake katika eneo hilo.

Weledi wa mambo wanaamini kuwa, hadi sasa Marekani imefeli kwa kiasi kikubwa katika siasa zake za kupenda kujitanua kuihusu serikali ya Pyongyang na badala yake imebakia ikitumia shinikizo na vitisho pekee dhidi ya nchi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!