May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kim awarudisha Yondani na Kessy Taifa Stars

Spread the love

 

KOCHA mkuu wa kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen ameita jumla ya wachezaji 43 watakao ingia kambini kuanzia tarehe 8 Machi 2021, huku akiwajumuisha kikosini mabeki Hassani Kessy pamoja na Kelvin Yondani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kikosi hiko kitaingia kambni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Kenya itakayopigwa Machi 16 na 18 2021, jijini Nairobi na baadae timu hiyo itasafiri kuelekea Equtorial Guinea kwa ajili ya mchezo wa kufuzu kombe la Mataifa Afrika (AFCON).

Mara ya mwisho kwa Hassani Kessy kucheza Taifa Stars ilikuwa baada ya kukamilika kwa michuano ya AFCON iliyofanyika nchini Misri Juni 2019, huku kikosi kikinolewa na Emannuel Amunike.

Kwa upande wa beki kisiki Kelvin Yondani ambaye aliataka kutundika daruga kuchezea Taifa Stars mara baada ya kukamilika kwa AFCON, lakini alirejeshwa na kuisadia timu hiyo kufuzu kwenye michuano ya CHAN iliyomalizika hivi karibuni nchini Cameroon mara baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Sudan.

Akitangaza kikosi hiko mbele ya wandishi wa habairi hii leo 26 Februari 2021, kwenye makao makuu ya shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) Poulsen alisema kuwa kigezo kikubwa alichotumia kuwaita wachezaji hao ni kucheza kwa moyo na kujitoa kwa jili ya nchi.

“Kwangu mimi sifa muhimu ni kutaka mchezaji mwenye moyo wa kuchezea kwa jili ya nchi yake, kwa kuwa hiki ni kitu muhimu, siku hizi unaweza kuwa na uwiano mzuri kwenye timu lakini usiweze kufikia malengo” alisema Kim Poulsen

Aidha Poulsen aliongezea kuwa malengo makubwa ya Taifa Stars ni kufuzu kwenye kundi lake kwa jili ya michuano ya AFCON hivyo anapenda kuwa na wachezaji wanaotaka kukua, kujifunza na kupata mafanikio.

“Nataka wachezaji wenye mtazamo mzuri, wanaotaka kukua, kujifunza na kupata mafanikio, mpira wa siku hizi sio wa mtu mmoja ni timu nzima ambayo inakaa pamoja na kitu hiki nimekiona kwa siku za hivi karibuni hapa Tanzania kwa baadhi ya timu za Ligi Kuu” aliongezea Kim Poulsen

Kikosi kamili hiko hapo chini.

error: Content is protected !!