January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kilwa watakiwa kuitosa CCM

Kamanda wa Chadema mkoa wa LIndi, Benedick Kimbache akihutubia katika ziara hiyo

Spread the love

WANANCHI wa mikoa ya Kusini wametakiwa kutobweteka kwa mafanikio madogo ya ujenzi wa barabara badala yake, wametakiwa kukiondoa Chama Cha Mapinduzi madarakani kwa kuichagua Chadema. Anaandika Mwandishi wetu…(endelea).

Akizungumza na wanakijiji wa Njianne huko Kilwa, Kasimu Bingwe- Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mtwara na Kaimu mwenyekiti wa Kanda mpya ya Kusini inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara, amesema Tanzania haipo huru kama watu wavyoaminishwa.

Amesema uhuru ni wananchi kufaidi matunda ya rasilimali zake. Bingwe amewatahadharisha wananchi kutoikumbatia CCM kwani kwa kufanya hivyo hawatapata uhuru wa kweli.

Bingwe ameonyesha masikitiko yake kwa uongozi uliopo madarakani kwamba wanawatawala watu mithiri ya utawala wa kikoloni.

“Sisi vyama vya upinzani tumesingiziwa mambo tofauti, ikiwa ni pamoja na kuitwa wahuni, sisi sio wahuni na wananchi wa Njianne msiyumbishwe kwa hilo kwani hata baba wa Taifa alipata kuitwa mhuni, lakini hao hao waliomuita muhuni ndio waliompokea kwa shangwe tulipopata uhuru,”amesema.

Bingwe ametolea mfano wa Chadema akisema ni sawasawa na mti wa mwembe unopigwa mawe kwa sababu ya matunda yake.

Katika ziara hiyo alisikitika kuona Watanzania wanaendelea kuikumbatia CCM, alihoji kwa nini waendelee kuipa nafasi ya kutawala wakati wanafahamu wamegeuzwa ndondocha.

Naye mweka nia ya ubunge kupitia tiketi ya Chadema kwa jimbo la Kilwa Kaskazini, Benedict Kimbache amewataka wananchi wa Kilwa Masoko kutumia umoja wao ili kuiondoa CCM iliyosababishia umasikini wa kutupwa.

Kimbache amewahakikishia wananchi wa Masoko kuwa endapo Chadema itaingia madarakani kupitia UKAWA, itakuwa na viongozi wenye uadilifu.

Akizungumzia kuhusu madini, Kimbache aliwataka wananchi kutothubutu kuiingiza CCM madarakani kwani neema ya mali asili waliyonayo hasa gesi ambayo wanaaminishwa inaweza kuondoa umasikini ifikapo mwaka 2025, inaweza isiwe hivyo.

error: Content is protected !!