December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kilosa wapewa elimu ya kusimamia rasilimani za umma

Wanafunzi wa shule ya msingi

Spread the love

WAKAZI wilayani Kilosa wametakiwa kufuatilia na kusimamia kikamilifu matumizi ya rasilimali za Umma hasa kwenye sekta ya elimu ili kuboresha miundombinu ya shule za msingi na sekondari na kukuza kiwango cha elimu mashuleni. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya kutoa elimu kwa jamii- Dira mkoani Morogoro, Erasmo Tullo alisema hayo wakati Shirika hilo likitoa elimu ya ufuatiliaji na usimamizi wa matumizi ya rasilimali za Umma sekta ya elimu ya msingi sambamba na Sekondari katika shule zilizopo ndani ya kata tano za wilaya hiyo kupitia ufadhili wa The Foundation For Civil Society (FCS).

Tullo alisema, kila mwenye dhamana ya kushikilia rasilimali za Umma anapaswa kuwa muwazi ili kuwezesha taarifa hizo kujulikana kwa kila mwananchi.

Aidha aliitaka jamii kuzingatia uwepo wa uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji kwa lengo la kupatikana huduma bora katika maeneo yao.

Hata hivyo Tullo aliwashauri wananchi wa wilaya hiyo, watapokuwa wanakaa kujadiliana na kuchangia masuala ya maendeleo ya sekta ya elimu wanapaswa kuangalia kama matumizi yanaendana na uhalisia wa fedha iliyokusanywa ili kuondokana na changamoto ya ubadhilifu inayorudisha nyuma maendeleo ya sehemu yoyote.

Alisema, ikiwa watajenga nidhamu ya kukiheshimu walichochangia watajikuta wanaongeza kasi ya maendeleo kwenye vijiji vyao ikiwemo kuboresha madarasa machakavu, kuhakikisha chakula kinapatikana shuleni, kumalizia miradi viporo, kujenga vyoo vipya, madarasa na pengine nyumba za walimu vyote vikiwa katika hali ya ubora.

Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mbamba, Msafiri Makau aliwaasa wanakijiji wenzake kuona haja ya kuamka na kufuata elimu waliyopewa na Dira kwani kufanya hivyo kutawasaidia kupunguza au kumaliza kabisa changamoto za elimu kijiji kwao.

Shirika la Dira linaendesha mradi wa kufuatilia na kusimamia matumizi ya rasilimali za Umma ukijikita kwenye sekta ya elimu ya msingi sambamba na Sekondari katika kata tano za wilaya ya kilosa ambazo Kilangali, Zombo, Mabwerembere, Ulaya na Tindiga.

error: Content is protected !!