May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kilio Katiba Mpya chatua UNHRC

Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu

Spread the love

 

ASASI za Kiraia nchini Tanzania, zimewasilisha kilio cha upatikanaji wa Katiba Mpya katika Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu (UNHRC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi tarehe 1 Aprili 2021, na Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa wakati akizungumza na wanahabari kuhusu Ripoti ya Tathimini ya Hali ya Haki za Binadamu nchini (UPR) katika kipindi cha miaka minne (2017-2020).

Olengurumwa amesema, kilio cha ufufuaji mchakato wa upatikanaji Katiba Mpya ni miongoni mwa masuala yaliyomo katika ripoti ya UPR, iliyowasilishwa Makao Makuu ya UNHRC, Geneva Usiwisi  tarehe 25 Machi 2021, ambayo Serikali ya Tanzania haijakamilisha michakato yake.

Olengurumwa amesema, ukamilishwaji wa mchakato huo ni miongoni mwa mapendekezo 133 ya UNHRC yaliyotolewa 2016, ambayo  Serikali ya Tanzania ilikubali kufanyia katika kipindi cha miaka minne.

“Kukamilika kwa mchakato wa katiba mpya, ni mapendekezo mojawapo ya 2016, Serikali ilisema watakamilisha. Lakini tunapokwenda kuripoti haijakamilisha, hiyo ndio tathimini yetu ambayo imepelekwa UNHRC Geniva, Uswisi.” amesema Olengurumwa.

MwanaAZAKI huyo amesema“Hivyo pendekezo la kukamilika kwa mchakato huo halikuguswa kabisa, sababu awamu hii ilikuwa kumalizia, awamu iliyopita ilikuwa ni kuuanzisha mchakato huo, ambapo Serikali ilitekeleza kwa kuuanzisha.”

Akielezea muhtasari wa ripoti hiyo, Olengurumwa amesema asimilia 89 ya mapendekezo hayo 133 yametekelezwa nusu, huku asilimia saba ya yakitekelezwa kwa asilimia 100, wakati asilimia 4 hayajatekelezwa kabisa.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga

Olengurumwa ametaja baadhi ya masuala yaliyotekelezwa kwa asilimia 100 kuwa ni, mapambano dhidi ya rushwa na ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), Anna Henga, ameishauri Serikali kukamilisha utekelezwaji wa mapendekezo hayo, ili kuimarisha hali ya haki za binadamu nchini.

“Huu ni mchakato wa hiari kutokana na uhuru wa nchi, hatuwezi kulazimishwa fanyeni, ila Tanzania ni moja wapo ya wanachama wa UN, tuna wajibu wa kuwajibika katika michakato ya umoja huo.

Kama tusipotekeleza ni aibu kwa Taifa, ni mchakato unachukuliwa kwa uzito wa hali ya juu,” amesema Henga na kuongeza:

“Faida ya kushiriki mchakato huo ipasavyo hali ya haki za binadamu itakuwa vizuri zaidi, mchakato huu serikali ingeupa kipaumbele.”

error: Content is protected !!