October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kilichosababisha kifo cha Mzee Akilimali chaanikwa

Spread the love

FAMILIA ya mwanachama wa siku nyingi na maarufu  ndani ya Klabu ya soko ya Yanga Ibrahim Akilimali, yaeleza kuwa ugonjwa wa saratani ndio uliosababisha kifo cha mzee huyo. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Kaimu Akilimali mtoto wa kwanza wa Mrehemu Akilimali ameiambia MwanaHALISI ONLINE  kuwa Baba yake amefariki kwa ugonjwa wa saratani ambao uligunduliwa  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

“Mzee alipangiwa kuhudhuria kliniki ya maradhi hayo na hata hivi alipangiwa arejee tena mwezi wa kwanza mwakani.

“Kuna wakati mikono  na miguu yake ilikuwa meupe tukadhani kuwa amepungua damu tukampeleka tena hospitali tukaambiwa damu imepungua akawa anakunywa dawa za kuongeza damu …kwa kuwa hali ya hewa ya Dar es Salaam haikuwa mzuri kwake tukampelekea nyumbani kwetu Bagamoyo kupumzika”

Kaimu amesema kuwa alipokuwa bagamoyo hali ya afya ilibadilika ndipo walipomfikisha kwenye Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo ambapo alitibiwa mpaka kufikia usiku wa kuamkia jana tarehe 14 Desemba 2019, alifariki dunia.

Mzee Akilimali amezikwa leo tarehe 15 Disemba 2019 Tandale jijini Dar es Salaam mbele ya msikiti ambao aliuasisi miaka ya nyuma, hiyo ikiwa ni moja ya usia aliouacha kwa watoto zake ya kuwa akifariki azikwe katika msikiti huo lakini mazishi yafanyike nyumbani kwao Bagamoyo.

Mzee Akilimali ni babu wa wajukuu 32 katika watoto wake wanne aliobahatika kupata. Watatu wa kiume na mmoja wa kike aliowazaa na wake zake watatu lakini kwa sasa ana wake wawili.

Maisha ya Mzee Akilimali kwa kifupi

Kaimu ameeleza kuwa Baba yake alikuwa mtu anayependa dini mpaka kufikia kuasisi msikiti wa Masjid Barakat  ulikuwepo Tandale kwa Mtogole.

Ameeleza kuwa alipenda pia mpira na pia alikuwa mwanasiasa licha ya kuwa msuluhishi kwenye jamii. Kaimu amesema kuwa kuondokewa kwa Baba yao huyo ni pigo kubwa.

Akilimali alizaliwa mkoani Kigoma mwaka na historia yake katika suala zima la soka ni kuwa ni mmoja wa aliyekuwa wapenzi na wanachama wa mwanzo kabisa wa Klabu ya Young African Sports Club, tangu mwaka 1956. ambapo aliwahi kutaja sababu kuu mbili zilizomfanya aipende Yanga kwa miaka 58 sasa.

Mosi, ni neno ‘Afrika’. Tangu zamani alikuwa akipenda kudumisha na kuutukuza Uafrika wake, kipindi hicho alikuwa mfuasi na mwanachama wa Chama cha Tanu (Tanganyika African National Union), ambacho baadaye kiliipatia Tanganyika uhuru wake mwaka 1961″.

error: Content is protected !!