July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kila la kheri Twiga, TFF wawapa mapato yote

Wachezaji wa Twiga Stars wakiwa katika mazoezi

Spread the love

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameitakia kila la kheri timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars) katika mchezo wake wa kesho wa marudiano dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (She-Polopolo) utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akiongea na wachezaji wa Twiga Star na benchi la ufundi katika chakula cha pamoja cha mchana leo katika hosteli za TFF zilizopo Karume, Rais Malinzi amesema watanzania wote wana matumaini na timu yao kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa marudiano.

Aidha Rais Malinzi amewaambia benchi la ufundi na wachezaji wa Twiga Stars kuwa pesa zote zitakazopatikana katika mchezo wa kesho baada ya makato ya Uwanja na VAT, wagawane kwa pamoja wachezaji na viongozi.

Naye Mgeni mualikwa Ryhs Torrington ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha Luninga cha Azam, alisema anaitakia kila la kheri Twiga Stars katika mchezo wao wa kesho, na kusema mechi hiyo itaonyeshwa moja kwa moja na Azamtv, hivyo waitumie vizuri nafasi hiyo kujitangaza kimataifa.

Kocha mkuu wa Twiga Stars Rogasian Kaijage na nahodha wake Sophia Mwasikili, wamewahakikishia ushindi katika mchezo wa kesho,  na kuwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuja kuwashangilia.

Twiga Stars ambayo katika mchezo wa awali iliibuka na ushindi wa mabao 4-2, inahitaji sare ya aina yoyote ili kuweza kufuzu kwa fainali za Michezo ya Afrika zitakazofanyika nchini Congo-Brazzavile mwezi Septemba.

error: Content is protected !!