July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kikwete kuongoza mkutano wa Lishe

Rais Jakaya Kikwete

Spread the love

RAIS Jakaya Kikwete, anatarajiwa kufungua mkutano ulioandaliwa na Chama cha wataaluma wa masuala ya Chakula na Lishe Tanzania (FONATA), ambao utajadili suala la udumavu kwa watoto nchini. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Mkutano huo, ambao umeandaliwa kwa ushirikiano wa Shirika la vyama vya masuala ya Chakula na Lishe Afrika (FONUS), utafanyika kuanzia Mei 24 hadi 29 mwaka huu, mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa Rais wa FONUS, Prof. Joyce Kinabo, lengo la mkutano huo ni kutoa fursa kwa wanasayansi wa masuala ya Lishe kubadilishana uzoefu kuhusiana na utekelezaji wa shughuli za lishe na mwelekeo wake.

Kinabo amesema, Tanzania pia ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa watoto waliodumaa kutokana na uhaba wa chakula bora kwa mama na mtoto kabla na baada ya kuzaliwa kwa mtoto.

Amesema, kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za mwaka 2015, imebainika kuwa zaidi ya watoto 2.7 milioni walio chini ya miaka 5 wamedumaa. Hivyo, utapia mlo bado ni miongoni mwa changamototo kubwa nchini.

“Licha ya jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali, kumekuwa na ushirikiano wa wadau na sekta mbalimbali kuhakikisha kuwa, upatikanaji wa lishe katika maeneo mbalimbali nchini unaongezeka kwa kutenga fedha maalumu.

“Kimsingi mkutano huu, unatazamiwa kutoa majibu mbalimbali ya mambo muhimu yamayohusiana na chakula na lishe yaliyoibuliwa na wataalamu wa lishe na wadau mbalimbali pamoja na watunga sera,” alisema.

Aidha, Kinabo ametoa wito kwa wakazi wa Arusha  kujitokeza kwa wingi haswa wanawake ili kuweza kupata elimu juu ya lishe bora ili kuepukana na tatizo hilo.

error: Content is protected !!