May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kikwete, Koroma wamaliza ubishi Zambia

Spread the love

RAIS mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na Rais mstaafu wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma, wamefanikiwa kumaliza utata ulijitokeza katika uchaguzi mkuu wa Zambia baada ya Edger Lungu, Rais aliyekuwa anatetea kiti chake kuangushwa. Anaripoti Gabriel Mushi…(endelea).

Kikwete alikuwa Mwangalizi Mkuu wa Jumuiya ya Madola wakati Koroma alikuwa Mwangalizi Mkuu wa Umoja wa Afrika – AU katika uchaguzi huo uliofanyika tarehe 12 Agosti, 2021.

Lungu aliyekuwa akitetea nafasi yake, alipata kura milioni 1.8 huku mpinzani wake Hakainde Hichilema ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani cha United Party for National Development (UNDP), akipata kura milioni 2.8 jambo ambalo hapo awali alikuwa amekataa kukubaliana matokeo hayo.

Hata hivyo, baada ya mazungumzo yaliyofanywa na Kikwete, Koroma pamoja na Rais mstaafu wa nchi hiyo, Rupia Banda sasa mambo ni shwari.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Lungu aliandika hivi; “Mapema leo (jana) Rais mteule Bwana Hakainde Hichilema na mimi tulifanya mkutano pamoja na Mwangalizi Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Rais wa zamani wa Tanzania, @jmkikwete na Mtazamaji Mkuu wa AU, Rais wa zamani wa Sierra Leone @ebklegacy. Tumekubaliana kujitolea kuweka masilahi ya Zambia mbele.”

Naye Hichilema naye aliandika hivi; “Nilikuwa na mkutano na Rais Lungu leo mchana mbele ya Marais Banda, Koroma na Kikwete. Wawili hao wa mwisho walikuwa sehemu ya ujumbe wa waangalizi wa AU kwa uchaguzi uliomalizika”.

error: Content is protected !!