May 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Kikwete, Kinana, Ndugai wamewakosea nini?’

Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete

Spread the love

 

TABIA ya kusemwa vibaya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete; Spika wa Bunge, Job Ndugai; Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama kumemkera Deo Sanga, Mbunge wa Makambako (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza bungeni leo tarehe 21 Aprili 2021, wakati wa mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa mwaka 2021/2022, Sanga amesema, tabia ya kuwasema wastaafu na wabunge hao ikomeshwe na kwamba, ikiachwa itasababisha sintofahamu.

Amesema, kwenye mitandao ya kijamii, viongozi hao wamekuwa wakinangwa huku mamlaka husika vikiangalia, amesisitiza kwa jambo hilo halipaswi kuachwa liendelee.

“Nani atafuata mheshimiwa spika? Hii ni hatari. Ni lazima tukemee kwa jambo ambalo linaweza kutugombanisha Watanzania, tukiliacha likaendelea, kesho kutwa hatujui atawekwa nani,” amesema.

Sanga amesema, Rais Kikwete amefanya kazi kubwa kwenye utawala wake, ametaka wanaomsema vibaya wamwanche apumzike huku akibainisha kazi kubwa iliyofanywa na Nape pia Kinana, Katibu Mkuu wa CCM wa zamani mwaka 2013-2015, ilikuwa ya kutukuka.

“Mheshimiwa Kikwete akapumzike, amefanya kazi yake vizuri, Kinana akapumzike. Nape wewe ni shahidi 2013 – 2015 wakati wa uchaguzi, Nape na Kinana walizunguka miaka mitatu kutafuta kura za CCM,” amesema.

error: Content is protected !!