March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kikwete, Cheyo kuwamwakilisha Rais Magufuli kuapishwa Mnangagwa

Spread the love

DK. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, anatarajiwa kumwakilisha Rais John Magufuli katika sherehe za kuapishwa wa Emmerson Mnangagwa, Rais Mteule wa Jamhuri ya Zimbabwe zitakazofanyika Jumapili tarehe 26 Agosti, 2018 katika uwanja wa michezo wa Taifa Mjini Harare. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa kwa vyombo vya habari leo tarehe 25 Agosti, 2018 na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Taarifa hiyo ya Ikulu imeeleza kuwa, Rais Magufuli amemtuma Dk. Kikwete kumwakilisha ambapo atafuatana na Phillip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM na John Cheyo, Mwenyekiti wa chama cha UDP.

Rais Mnangagwa ataapishwa kesho kuongoza Zimbabwe baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 30 Julai, 2018 ikiwa anapokea kijiti kutoka kwa Robert Mugabe aliyekuwa Rais wa nchi hiyo.

error: Content is protected !!