June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kikwete: Barabara za vijijini zitainua uchumi

Spread the love

RAIS Jakaya Kikwete amewataka viongozi wa serikali za mitaa kuhakikisha kuwa wanajenga barabara maeneo ya vijijini ili kuchochea maendeleo na kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi zilizoko katika maeneo hayo. Anaandika Ferdinand Shayo, Arusha … (endelea).

Kikwete amesema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa Viongozi wa serikali za mitaa (TAMISEMI) uliowakutanisha wakuu wa mikoa, wilaya na Wakurugenzi kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa ubora wa kazi na barabara endelevu.

Rais Kikwete amesema kuwa ujenzi wa barabara vijijini utafungua milango ya maendeleo vijijini na kubadilisha maisha ya watu wengi.

Pia Rais Kikwete amewataka viongozi wa serikali za mitaa kuwa waaminifu katika kusimamia mfuko wa barabara ambao umefikia kiasi cha shilingi 800 bilioni ili mfuko huo uweze kuwahudumia watanzania badala ya kuwanufaisha watu wachache.

“Fedha hizi za mfuko wa barabara zikitumika vizuri zitapunguza matatizo ya miundombinu ya barabara yanayozibiri sehemu nyingi nchini,” amesema Kikwete.

Kwa upande wake, Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia amesema kuwa wizara yake imeanzisha idara kamili ya Miundombinu ambayo itafanya ukaguzi na kuzuia hasara inayotokana na ujenzi wa barabara chini ya kiwango.

Ghasia amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya fedha inayokwamisha ukarabati wa barabara za mitaa ambazo husadia upanuzi wa miundombinu katika maeneo mbalimbali.

Naye Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Jumanne Safini amesema kuwa wizara hiyo inakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa rasilimali za kutosha hali inayosababisha viwango duni vya barabara vinavyotokana na kukosekana kwa usimamizi na ukaguzi hivyo kutopata barabara endelevu.

error: Content is protected !!