January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kikwete atoa siri ya kushuka kwa thamani ya shilingi

Spread the love

RAIS Jakaya Kikwete ameeleza sababu iliyosababisha kushuka kwa thamani ya sarafu ya Tanzania kuwa nikutokana na watanzania kununua bidhaa nje ya nchi. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa akizindua majengo ya Benk Kuu la Tanzania (BOT) tawi la kanda ya kati, jengo la Hazina na jengo la Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali CAG mjini hapa.

Kikwete amesema kuwa watanzania wanaonunua bidhaa nje ya nchi ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa kushusha sarafu ya Tanzania.

“Sasa yatupasa kulidhibiti tatizo hili ili tuirudishe sarafu yetu kwenye hadhi yake na Jukumu kubwa la kuipandisha sarafu yetu wanayo Benk Kuu ya Tanzania (BOT),”amesema Kikwete.

“Lakini na sisi watanzania tupende vya kwetu, tununue bidhaa nchini kwetu na mimi naamini kwamba tukifanya hivi tutasaidia kuipandisha sarafu,”amesema.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha, Saada Mkuya amesema ujenzi wa majengo hayo ni utekelezaji wa mpango wa serikali ya kujenga na kuendeleza makao makuu ya serikali kuwa Dodoma.

Amesema utekelezaji wa miradi hiyo ilianza tangu mwaka 2010 kwa ujenzi wa jengo la Benk Kuu ya Tanzania, mwaka 2011 jengo la hazina mwaka 2012 ujenzi wa jengo la ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na yalikamilika kwa wakati.

Mkuya amesema makusudio ya ujenzi yalilenga kutekeleza maagizo ya serikali ya kujenga na kuendeleza makao makuu ya serikali kuwa Dodoma na kutimiza lengo la wizara la kuhakikisha kuwa ofisi zote za Hazina ndogo zilizopo mikoani zinapata majengo kwa matumizi ya tasisi zote zilizopo chini ya wizara.

“Kukamilika kwa mradi huu kumeleta unafuu mkubwa wa watumishi wa Hazina na pia kwa taasisi mbalimbali za serikali ambazo hazina ofisi hapa Dodoma na mpaka sasa jumla ya wizara tano zimepatiwa nafasi katika jengo la Hazina ,” amesema Mkuya.

error: Content is protected !!