July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kikwete atakiwa kuingilia kati BVR

Rais Jakaya KIkwete (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipiumba

Spread the love

RAIS Jakaya Kikwete, ametakiwa kuhakikisha wananchi wote wanaandikishwa katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.

Lipumba amesema “Natoa wito kwa Rais Kikwete. Ahakikishe wananchi wote wanaandikishwa na kupata haki ya kupiga kura”.

“Asichukue taarifa za juu juu. Aende aombe idadi ya wananchi wangapi wameandikishwa. Atazame ni watu wangapi wameandikishwa kila kata kwa uwiano wa idadi ya wapiga kura waliokadiliwa katika maeneo hayo. Hili ndio suala la kusimamia,” amesema Lipumba.

Lipumba amesema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inapaswa kuacha kutumia fedha kwa mambo ambayo hayahitajiki kwa sasa, ikiwemo kugharamia mafunzo na tenda za kutoa huduma kwa ajili ya kura ya maoni.

Badala yake NEC ifike kuhakikisha wananchi wanaandikishwa katika dafatari la kudumu la mpiga kura kwa kutoa elimu kwa kuwa kwa sasa hakuna sheria inayosimamia kura ya maoni ambapo ya awali imekwishavunjwa.

“Nimepata wasisi jana ambapo Jestina Mhagama alikuwa anazungumzia bungeni kuwa serikali itaweza kuandikisha wapiga kura 17 milioni. Wakati tuna wapiga kura zaidi ya 24 milioni,” ameongeza Lipumba.

Lipumba ameeleza kuwa zoezi la uandikishaji bado halijafanikiwa kwa kiwango kikubwa. Kwa mfano katika kijiji cha Milonde, wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wananchi walioandikishwa kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) ni 920 kati ya 2260 wenye sifa ya kuandikishwa.

“Mfano mwengine ni katika kijiji cha Mchemo ‘A’, kata ya Mchemo, wilaya ya Newala kadi ya kuandikishwa inaelezwa ni ya Kata ya Mpwapwa. Hivyo ni watu 31 walioandikishwa kati ya watu 359 wenye sifa ya kuandikishwa,” anafafanua Lipumba.

Lipumba ameeleza kuwa licha ya kuwepo kwa vifaa 4700 vinavyotumika kuandikisha lakini vingine havitumiki kwa sababu NEC imeshidwa kuwalipa waandikishaji zaidi huku wale wanaolipwa wakiambulia posho ya Sh. 100,000 kwa wiki. Fedha ambazo hazitoshelezi kwa mahitaji ya kuishi huko.

Aidha, Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho, Magdalena Sekaya ambaye ametembelea maeneo yanayoendelea na uandikishaji amesema “Wananchi wanaona wananyimwa haki yao. Taifa na serikali isipoangalia yataibuka machafuko”.

error: Content is protected !!