Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kikwete alivyomzungumzia Magufuli, ampongeza Rais Samia
Habari za Siasa

Kikwete alivyomzungumzia Magufuli, ampongeza Rais Samia

Rais John Magufuli akiwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
Spread the love

 

RAIS mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema, kifo cha aliyekiwa Rais wa Taifa hilo, Dk. John Pombe Magufuli, kimewashtua wengi nani pigo kubwa. Anaripoti Matrida Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Kikwete aliyekuwa Rais kati ya mwaka 2005 hadi 2015 kisha akamwachia kijiti Dk. Magufuli, imemchukua takribani siku mbili, kuzungumzia kifo hicho.

Dk. Magufuli (61), alifikwa na mauti saa 12 jioni ya Jumatano tarehe 17 Machi 2021, akiwa Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam, akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mfumo wa umeme wa moyo.

Mwili wake, utazikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita, Alhamisi ijayo tarehe 25 Machi 2021.

Kufuatilia kifo hicho, aliyekuwa makamu wake, Samia Suluhu Hassan, ameapishwa leo Ijumaa tarehe 19 Machi 2021, katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Kikwete.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Kikwete ameandika “Nimepata tabu kuandika kwa kifupi kuelezea simanzi na masikitiko yangu kwa msiba mkubwa ulioukumba nchi yetu kwa kuondokewa na mpendwa wetu Mheshimiwa Rais John Magufuli.”

“Nimelazimika kuyaambatisha hapa chini. Mwenyezi Mungu amuweke mahala pema, peponi,” amesema

Undani wa alichokiandika ikiwa ni pamoja na kutoa nasaha kwa Rais mpya Samia, soma hapa chini;

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

Habari za Siasa

PIC yaishauri Serikali kuanzisha mfuko wa uwekezaji kusaidia mashirika ya umma

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

error: Content is protected !!