January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kikwete akinzana na Profesa Baregu

Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Prof. Mwesiga Baregu

Spread the love

WAKATI Rais Jakaya Kikwete amejitamba kuwa Katiba Inayopendekezwa ni bora, aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Profesa Mwisigwa Baregu, amekinzana naye akisema kuwa asilimia 85-95 ya maoni ya wananchi yalinyofolewa na Bunge Maalum la Katiba (BMK). Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Akuzungumza jioni hii, katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma wakati akihutubia Bunge la 10 kabla ya kulivunja, Rais Kikwete amesema japo maoani kuhusu katiba inayaopendekezwa hayakupatikana lakini katiba inayopendekezwa ni bora na itasaidia kuboresha muungano wa serikalia mbili.

“ …natoa shukrani nyingi kwa bunge….kura ya maoni haijafanayika. Katiba inayopendekezwa ni bora.” Amesema Kikwete.

Kauli hiyo ya rais inapingana na kauli aliyoitoa Prof. Baregu jana jijini Dar es Slaam wakati akichangia mada katika kongamnao la kujadili “amani, utulivu, uchaguzi mkuu wa mawaka huu na uongozi wa awamu ya tano”.

Katika kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere Prof. Baregu amesema , “Asilimia 85-95 ya maoani ya wananchi katika Rasimu ya Katiba Pendekezwa yalinyofolewa na Bunge Maalum la Katiba,”

“Wabunge wa Bunge Maalum wakaanza kujenga mitafaruku na misingi ya wananchi kutotii hiyo katiba mnayoitaka. Bahata mbaya au kwa makusudi likaja suala ala serikalia mbili,” amesema Baregu.

Baregu amesema kimsingi Bunge Maalum la Katiba lilipaswa kuendeleza mchakatao wa Katiba mpya na sio kuigiza upya maoani ambayo hayakupendekezwa na wananchi.

error: Content is protected !!