Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kijana mbaroni kwa kumkata kichwa dada’ke mjamzito
Kimataifa

Kijana mbaroni kwa kumkata kichwa dada’ke mjamzito

Spread the love

Polisi katika jimbo la Maharashtra – Magharibi mwa India wamemkamata kijana anayeshukiwa kumkata kichwa dadake mkubwa aliyekuwa mjamzito. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mwanamke huyo (19), alikuwa ameolewa na mwanamume bila idhini ya familia yake, maofisa wa polisi wa eneo hilo walisema.

Alikuwa akiwatengenezea kaka na mama yake chai aliposhambuliwa kwa mundu. Kijana huyo na mama yake kisha walijisalimisha kwa polisi.

Polisi wanashuku kuwa pia walipiga picha ya selfie na kichwa cha mwanamke huyo.

Ndugu huyo alipelekwa rumande kwa watoto baada ya wakili wake kusema kwamba alikuwa na umri wa chini ya miaka 18.

Hata hivyo, Ofisa mmoja wa polisi alisema wangepinga dai hili kortini kwa vile wamepata cheti kinachoonyesha kuwa ni mtu mzima. Mama yao aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi.

Kisa hicho kilitokea katika wilaya ya Aurangabad, BBC Marathi iliripoti.

Mwathiriwa alitoroka Juni na kuolewa na mpenzi wake baada ya familia yake kupinga uhusiano wao.

Ingawa wote wawili walikuwa wa tabaka moja, familia yake haikumkubali kwa vile familia yake ilikuwa maskini kuliko yao.

Mwanamke huyo hakuwasiliana na familia yake sana baada ya ndoa yake lakini mama yake alimtembelea wiki moja kabla ya mauaji. Polisi walisema alijua kwamba binti yake alikuwa mjamzito.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

Habari za SiasaKimataifa

Rais Faye amteua aliyekuwa mfungwa mwenzie kuwa waziri mkuu

Spread the loveRais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteua Ousmane Sonko...

error: Content is protected !!