September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kijana mbaroni kwa kumbaka mama yake mzazi

Spread the love

 

MATUKIO ya ukosefu wa maadili mkoani Dodoma yamezidi kuutikisa mkoa huo baada ya Jeshi la Polisi mkoani humo kumnasa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 30 kwa tuhuma za kumbaka mama yake mzazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma …  (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 22 Disemba, 2021 Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga amesema tukio hilo limetokea wilayani Kondoa.

Aidha, amesema katika operesheni waliyoifanya hivi karibuni pia walimkamata Babu mwenye umri wa miaka 61 kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka 11.

Amesema mjukuu huyo anayesoma darasa la nne, wote pamoja na babu yake ni wakazi wa Kongwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga

Pia ameongeza katika operesheni hiyo pia wamemkamata baba mwenye umri wa miaka 30 ambaye ametuhumiwa kumuingilia kinyume na maumbile mwanaye mwenye  umri wa miaka minne.

Amesema kutokana na matukio hayo ni dhahiri vitendo vya ukatili uliokithiri vimeendelea kushamiri mkoani humo hivyo ni vema jamii kurejea kwenye maadili.

“Lakini watuhumiwa wote tumeshawakamata na kwa ajili ya taratibu za kuwafikisha mahakamani,” amesema.

error: Content is protected !!