Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Habari Kijana afyatua risasi na kuua watu 10
HabariKimataifa

Kijana afyatua risasi na kuua watu 10

Spread the love

KIJANA mmoja kutoka mji wa Buffalo, New York anayefahamika kwa jina na Payton Gendron mwenye umri wa miaka 18, amefyatua risasi kwa makusudi na kuwauwa watu 10,katika eneo waliopo watu weusi. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa mitandao (endelea).

Mshukiwa Poyton Gendron, alisafiri kwa zaidi ya kilometa 320 (maili 200) kufanya shambulio hilo, na kuwauwa watu 10 katika duka la jumla huko New York, shambulio hilo amelifanywa kwa makusudi katika eneo waliopo watu weusi, polisi wanasema.

Rais wa Marekani Joe Biden amezungumzia juu ya mauaji hayo,yaliyochochewa na ubaguzi wa rangi katika mji wa Buffalo.

Biden aliuambia umati wa watu kuwa yeye na mke wake,Dr Jill wanawaombea waathiriwa, wa shambulio hilo, na kwamba ‘’chuki imeendelea kuwa doa kwenye roho ya Marekani.’’

Hata hivyo, shambulio hilo, linachunguzwa kama kitendo cha uchochezi wa ghasia za ubaguzi wa rangi.

Meya   wa mji wa Buffalo, Byron Brown amesema mshukiwa huyo alilenga kuchukua maisha ya watu weusi wengi, hata hivyo kumekuwa na maswali yakiulizwa kuhusu jinsi alivyofanya shambulio hilo, wakati kijana huyo alikuwa tayari anachunguzwa na mamlaka husika.

Gendron awali alitishia kufanya shambulio la risasi katika shule yake ya sekondari mwezi juni mwaka uliopita, afisa wa usalama aliliambia shirika la habari la Associated Press lakini alifanyiwa uchunguzi wa afya ya akili baadaye.

Aidha, maeneo mengine ambayo mashambulio yaliyotokea ambako yalichochewa na ubaguzi wa rangi,wenye itikadi kali za mitandaoni wamefanya itikadi zao kuwa kali na za hatari kiasi cha kuua.

Mashambulizi hayo, katika mji wa Buffalo, ni sawa na washambuliaji wa awali waliopeperusha moja kwa moja mtandaoni tukio hilo la ghasia na kuacha kile kinachoitwa,’’manifeso’’ mtandaoni ilielezea kwa kina kuwa imani zake za itikadi kali na ilijaa takwimu bandia, thana potofu na utani wa mtandaoni kwa njia ya mchoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Ramaphosa akiri tatizo la umeme Afrika Kusini kuathiri sekta ya madini

Spread the love  RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema tatizo la...

Kimataifa

Idadi ya vifo tetemeko la ardhi yafikia 9000

Spread the love  IDADI ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi Uturuki: Vifo vyaongezeka hadi 4,800

Spread the love  Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko lililotokea jana Jumatatu...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi laua watu 300 Uturuki, Syria

Spread the love  WATU  300 wamefariki dunia katika tetemeko kubwa la ardhi...

error: Content is protected !!