August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kigwangalla: sina ‘bifu’ na Dk. Mwaka

Spread the love

HAMISI Kigwangalla Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee amesema, hana mgogoro binafsi na tabibu Juma Mwaka, mmiliki wa Fore Plan kituo cha afya kilichofungiwa na serikali hivi karibuni, anaandika Pendo Omary.

Dk. Kigwangalla amesema matukio ya kukitembelea mara kwa mara na kukikagua kituo cha tabibu Mwaka ambaye ni maarufu kwa jina la Dk. Mwaka ni sehemu ya majukumu yake kama naibu waziri wa afya na siyo ugomvi binafsi baina yao.

“Juma Mwaka hajawahi kuwa rafiki wala adui yangu. Sina ugomvi binafsi na yeye na ninafanya kazi ya kusimamia Sheria ya tiba asili na tiba mbadala,” ameandika Kingwangalla katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook na kuongeza;

“Naithamini tiba asili na tiba mbadala ndiyo maana nimeongoza wizara yangu kufanya mapinduzi makubwa kwenye eneo hili, tumeweka utaratibu mzuri na rahisi zaidi wa kusajili watoa huduma, dawa zao na wasaidizi wao pia tuna mikakati ya uanzishwaji viwanda vya dawa za tiba asili na tiba mbadala.”

Dk. Kigwangalla amesema Mwaka anapaswa kujibu juu ya uhalali wa kutunza maboksi 200 ya dawa, magunia zaidi ya 10 ya dawa za tiba asili na tiba mbadala ilihali amefutiwa usajili huku pia dawa za tiba ya kisasa zikikutwa kwenye eneo lake.

“Alikuwa na uhalali gani wa kuendelea kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa wateja wake wafuate dawa ili wasikatishe dozi? Yupo juu ya Serikali? Juu ya sheria? Ama anadhani anaweza kuidhihaki na kuiogofya Serikali?” amehoji Kigwangalla.

error: Content is protected !!