July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kigwangalla awageukia wahamasisha ushoga

Spread the love

JAMES Wandela Ouma Kiongozi wa Shirika la LGBT Voice Tanzania anatuhumiwa kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja “ushoga” kupitia shirika hilo, anaandika Pendo Omary.

Katika taarifa iliyotolewa na Dk. Hamis Kigwangalla Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema shirika la LGBT chini ya uongozi wa Ouma limekuwa likitumia mitandao ya kijamii kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja jambo ambalo halivumiliki.

Aidha, Kigwangalla amemtaka Ouma kufika katika ofisi yake  ifikapo kesho saa 3.00 asubuhi akiwa na nyaraka halisi za usajili ikiwemo cheti cha usajili, katiba na orodha ya wanachama, taarifa ya miradi inayotekelezwa na shirika hilo, walengwa vwa miradi, wafadhili na wadau wanaoshirikiana nao.

“Ikumbukwe kwa kushidwa kufanya hivyo, kutapelekea kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Pia napenda niombe jamii kutoa taarifa kwa mamlaka zinazosimamia sheria pale ambapo wanabaini vikundi vya watu, mtu au taasisi zinahamasisha mapenzi ya jinsia moja,” amesema Kigwangalla.

error: Content is protected !!