August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kigwangalla atoa siku 90 kuboreshwa chumba cha upasuaji 

Dk.Hamisi Kigwangalla, waziri wa Maliasili na Utalii

Spread the love

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dk. Hamis Kigwangala ametoa miezi mitatu  kwa halmashauri ya mji wa Kahama kuhakikisha inafanya ukarabati wa chumba cha upasuaji katika hospitali ya mji wa  Kahama, anaandika Mwandishi Wetu

Ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kutembelea baadhi ya sehemu zinazotoa huduma za afya.

Akiwa hospitalini hapo Dk.  Kigwangala  amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kahama, Anderson Msumba kuhakikisha  anasimamia kazi hiyo kwa weledi ili  liweze kufanikiwa.

Pia amemtaka Mkurugenzi kuhakikisha anafanya marekebisho katika chumba cha kujifungulia akina mama wajawazito.

error: Content is protected !!