August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kigwangalla afungia kliniki za tiba asilia

Spread the love

SERIKALI imesitisha huduma za tiba asili zitolewazo na Kiliniki za Kikorea, Maibong Sukidar Medical na Korea Medical Clinic zilizopo Jijini Dar es Salaam kwa kosa la kutokuwa na kibali kwa zaidi ya miaka nane pia kuchanganya tiba asili na za kisasa na mbadala bila ya idhini kutoka baraza la usajiri la tiba asili nchini, anaandika Regina Mkonde.

Hatua ya kufungwa kwa kliniki hizo imechukuliwa leo baada ya Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kufanya ziara ya kushtukiza kukagua wa vibali na huduma zitolewazo katika kiliniki hizo.

Kigwangalla amezitaja sababu zilizopelekea kufungwa kwa Kiliniki ya Korea Medical ambazo ni

Kutibu magonjwa ambayo hazikupewa kibali kutoka serikalini, kuhifadhi dawa ambazo hazihusiani na magonjwa inayotibu ndio sababu zilizosababisha kliniki hizo kufungwa.Hiyo ni kwa Mujibu wa Kigwangalla

“Kliniki hii ninaamuru ifungwe kwa makosa matano ikiwemo kosa la kuchanganya tiba asili na kisasa, kutokuwa na kibali, usajili halali, matabibu wake hawajui lugha ya Kiswahili na au kiingereza, usajili ulimtaka kuajiri tabibu wa kitanzania ambaye hapa hayupo,” amesema Kigwangalla.

Amesema kliniki hiyo inatumia dawa kali za maumivu, usingizi, uzazi wa mpango, sindano na dripu.

Kigwangala amemwamuru msajili wa hospitali binafsi kufanya uchunguzi ili kubaini hizo dawa zilikuwa zinafanya kazi gani.

Zainab Sahabani ni mgonjwa anayetibiwa katika kliniki hiyo alipoongea na MwanaHALISI Online alithibitisha kuwa alitibiwa ugonjwa wa Athma na kwamba leo alikwenda kumalizia matibabu yake kabla Kigwangalla kuweka bayana kuwa kiliniki hiyo iliruhusiwa kutibu magonjwa ya ngozi na si vinginevyo.

Aidha, Kigwangalla ameeleza sababu ya kufungwa Kliniki ya Maibong ni pamoja na kutokuwa na kibali kwa zaidi ya miaka minane, kuchanganya tiba asili na kisasa na kutoplekea vyeti vya matabibu wake kama serikali ilivyomtaka kuvipeleka toka mwaka 2008.

“Kiliniki hii haina kibali walichonionesha ni barua walizoandika za kuomba kibali kutoka serikalini na kwamba serikali iliwaambia kupeleka vyeti vya matabibu wake jambo ambalo hawajalifanya hadi sasa,” amesema.

“Baraza la usajili tiba asili lifungie kliniki hadi itakaporekebisha nyaraka zake pamoja na kufanyiwa uchunguzi kama inakidhi vigezo vya kutoa huduma ya tiba asili na mbadala,” amesema.

Kigwangalla ametoa agizo kwa baraza la usajiri la tiba asili nchini kuzifungia kliniki hizo hadi zitakapofuata utaratibu, pia ameitaka idara ya uhamiaji kuchunguza vibali vya makazi na ufanyaji kazi nchini.

error: Content is protected !!