July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kigoma mbioni kupewa ardhi ya kilimo

Mbunge wa Kasulu mjini Mosesi Machali

Spread the love

WANANCHI wa Kijiji cha Kagera, Nkanda katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wameandaliwa utaratibu maalumu wa kupewa ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo, bunge lilielezwa jana. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Akijibu swali la Mbunge wa Kasulu mjini Mosesi Machali (NCCR- Mageuzi), Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Agrrey Mwanri, amesema wananchi hao wamepatiwa ardhi katika maeneo ya vijiji vingine ambako kulionekana kuwa na akiba ya ardhi.

Katika swali lake Machali, alitaka kujua ni sababu gani zinazokwamisha kushughulikiwa agizo la Waziri Mkuu la kuwapatia ardhi wananchi wa Kijiji cha Kagera Nkenda ambao waliondolewa kupisha Hifadhi ya Kagera Nkanda.

Aidha mbunge huyo alipinga kauli ya serikali kwamba, wananchi hao wamepatiwa ardhi kwani bado kuna malalamiko mengi kutoka kwa ananchi na majibu ya Serikali yamekuwa si ya kutoa matumaini.

Naibu Waziri alikiri kuwa, Waziri Mkuu kwa nyakati tofauti alitoa tamko kuwa wananchi wa eneo hilo watapatiwa ardhi mbadala ili kuwasaidia kuendesha shughuli zao za kilimo.

“Eneo linalozungumziwa hapa ni eneo linalotambuliwa kisheria kuwa ni hifadhi ya Misitu ya Makere Kusini ambako baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kagera Nkenda waliingia kinyume cha sheria kwa ajili ya kilimo,”amesema Mwanri.

Alitoa mfano kwa vikundi ambavyo vimeombwa na vitapatiwa ardhi katika maeneo mengine ni kikundi cha UWT walioomba ekeri 200 ambao walipewa kijiji cha Katanga,Mrubona waliomba ekari 1,500 na kupewa kijiji cha Titye na Kilimo kwanza waliomba 15,600 ambao walipewa Kijiji cha Kitanga.

Wengine ni Kijiji cha Tukomboane ekari 200 walipewa Mwanga B, Juhudu Tujenge Taifa ekari 9,900 ambao walipewa Rungwe mpya na Kaguruka.

error: Content is protected !!