Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Kigogo wa TAKUKURU aburuzwa kizimbani kwa uhujumu uchumi
Habari Mchanganyiko

Kigogo wa TAKUKURU aburuzwa kizimbani kwa uhujumu uchumi

Spread the love

TAASISI ya Kuzuiya na Kupambana na Rushwa  (Takukuru)  imemburuza kortini Kulthum Mansoor, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini  kwa kudaiwa kughushi na kujipatia kiasi cha Sh Bil 1.4. Anaripoti  Faki Sosi…(endelea).

Wakili wa Serikali Mkuu, Wankyo Simon mbele ya Hakumu Mfawidhi, Kelvin Mhina amemsomea mashtaka ya utakatishaji fedha mtuhumiwa huyo.

Shitaka la kwanza ni kughushi ambapo Bi. Kulthum alidaiwa kuwa, ametenda kosa hilo katika tarehe tofauti, kati ya Januari 2013 na Mei  2018 ndani ya Ofisi za Takukuru.

Kwenye shitaka hilo, Bi. Kulthum anadaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kati ya  tarehe tofauti ndani ya  Januari 2012 na Mei 2018, Upanga jijini Dar es Salaam  akiwa Ofisa wa Takukuru kwa njia za udanganyifu.

Imeelezwa kuwa, alijipatia Sh. 5 Milioni kama malipo ya kiwanja kwa njia ya udanganyifu.

Shitaka la pili ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo Januari 2012 na Mei 2018, Upanga, Dar es Salaam kwa njia za udanganyifu, alijipatia Sh. 5 Milioni kutoka   kwa  mtumishi mwenzake, Alex Mavika kama malipo ya kiwanja.

Shitaka la tatu, ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Mtuhumiwa anadaiwa  kati ya Januari 2012 na Mei 2017 Upanga, jijini Dar es Salaam kwa njia za udanganyia ulijipatia Sh. 5 Milioni, kutoka kwa mtumishi mwenzake Wakati Ndege malipo ya kiwanja ukidanganya kuwa yeye ni mmliki wa kiwanha hiko jambo ambalo sio kweli.

Kosa la  nne  pia ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu inadaiwa kati Januari 2012 na Mei 2017 Upanga jijini Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa Takukuru kwa njia za udanganyifu ulijipatia  Sh. 7 Milioni kutoka kwa mtumishi mwenzake Gogo Migutah  kama malipo ya kiwanja kilichopo kijiji Ukuni cha Bagamoyo ukidanganya kuwa ww ni mmliki wa kiwanja hiko jambo ambalo sio kweli.

Kosa la tano  Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu  ambapo inadaiwa mtuhumiwa kutenda kosa hilo kati Januari 2012 na Mei 2017 upanga jijini  Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa Takukuru kwa njia za udanganyia ulijipatia Sh7 Milion kutoka kwa mtumishi mwenzake Ekwabi Majungu kama malipo ya kiwanja kilichopo kijiji  cha Ukuni  Bagamoyo ukidanganya kuwa yeye ni mmliki wa kiwanja hiko jambo ambalo sio kweli.

Kosa la sita mtuhumiwa anadaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kati Januari 2012 na Mei 2017 upanga jijini Dar es Salaam akiiwa mwajiriwa wa Takukuru kwa njia za udanganyifu alijipatia  Sh.7 Milioni kutoka kwa mtumishi mwenzake John Sangwa  kama malipo ya kiwanja kilichopo kijiji cha Ukuni wilani Bagamoyo ukidanganya kuwa yeye ni mmliki wa kiwanja hiko jambo ambalo sio kweli.

Kosa la saba, Bi Kulthumu anashitakiwa  kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo kati Januari 2012 na Mei 2017 Upanga jijini Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa Takukuru kwa njia za udanganyia alijipatia Sh. 5 Milioni kutoka kwa Rose Sigela  kama malipo ya kiwanja kilichopo kijiji cha Ukuni Bagamoyo ukidanganya kuwa ww ni mmliki wa kiwanja hiko jambo ambalo sio kweli.

Kosa la nane utakatishaji fedha ambapo mtuhumiwa  anakabiliwa kwa kosa hilo analodaiwa kutenda kati   Januari 2013  na Mei 2018 ambapo inadaiwa kuwa ametakatisha kiasi cha Sh.1.4  Bilioni wakati akijuwa kuwa fedha hizo ni zao la fedha haramu za kughushi .

 

Wakili Wankyo amedai Mahakamani hapo Upelelezi haujakamilika ameomba terehe ya kutajwa kwa shauri hilo.

Hakimu Mhina ameahilisha shauri hilo mpaka tarehe 12 Aprili mwaka huu na kwamba Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo .

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

error: Content is protected !!